TFF YASOGEZA MBELE USAJILI SIKU MBILI
Wakati TFF ilikuwa ifunge usajili wa Ligi Kuu Bara usiku huu,
taarifa inasema siku mbili zimeongezwa.
Kuna taarifa Shirikisho hilo limeamua kuongeza siku mbili za
usajili sasa utafungwa tena Ijumaa saa 6 usiku.
“Kuna taarifa kwamba usajili umesogezwa mbele, tumepata taarifa
kupitia simu,” alieleza kiongozi mmoja wa klabu usiku huu.
Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa tayari Yanga na Simba
zilishawasilisha majina ya wachezaji wao watano wa kigeni.
Yanga iliwasilisha majina ya Wanyarwanda wawili (Mbuyu Twite na
Haruna Niyonzima), Wabrazil wawili (Jaja&Coutinho) na Hamis Kiiza huku
ikiwa imemtema Okwi.
Wakati Simba iliwasilisha majina ya Wakenya wawili (Modo
Kiongera&Donald Musoti), Warundi wawili (Amissi Tambwe&Peirre Kwizera)
na Mganda, Joseph Owino.
Bado haijajulikana sababu hasa za TFF kuamua kusogeza mbele kwa
siku mbili usajili huo.
Post a Comment