MAITI YA MWANAMKE YAZUA KIZAA ZAA GEITA,YAZIKWA KI- EBOLA EBOLA
Maiti ya mwanamke mmoja Bertha Boniphace(23)mkazi
wa kijiji cha Katoro Kata ya Katoro Wilaya na Mkoa wa Geita mwenye
dalili za ugonjwa wa Ebola imeutikisa mji wa Geita kiasi cha wakazi wa
mji huo kuhofia kushikana mikono wakihofia kuambukizwa.
Hatua
hiyo imekuja baada ya mwanamke huyo kufariki dunia akiwa katika
hospitali ya Wilaya ya Geita na ndugu kunyimwa mwili wake kwenda kuuzika na badala yake mwili huo kuzikwa na Serikali.
hospitali ya Wilaya ya Geita na ndugu kunyimwa mwili wake kwenda kuuzika na badala yake mwili huo kuzikwa na Serikali.
Baada
ya serikali kugoma kutoa mwili wa mwanamke huyo kwa ndugu zake ili
wakauzike,mvutano mkali ulitokea kati ya Uongozi wa Hospitali ya wilaya
ya Geita,na ndugu wa marehemu huyo ndugu hao wakipinga mwili wa marehemu
kwenda kuzikwa na serikali bila kutoa heshima zao za mwisho.
Kufuatia
hali hiyo walinzi wa Hospitali waliamuliwa kuwaondoa eneo hilo ndugu wa
Marehemu waliokuwa wamefurika wakitaka kujua sababu ya wao kuzuiliwa
kuona mwili wa marehemu bila kupewa taarifa sahihi za ugonjwa
uliosababisha kifo cha ndugu yao.
Nusura
walinzi na ndugu wa marehemu warushiane ngumi na watu hao ambao
walikuwa wamefura hasira na baadaye walinzi hao ambao hawakuwa na siraha
waliamua kuokota mawe na kuanza kuwarushia ndugu wa marehemu hali
iliyosababisha ndugu wa marehemu kutimua mbio.
Baadaye mwili wa marehemu ulitolewa kwenye Chumba maalumu cha hospitalini hapo kwenda kuzikwa na halmashauri ya Geita.
Msafara
wa kwenda kuzikwa kwa mwili wa marehemu katika Makaburi ya Mkoani Mjini
Geita uliongonzwa na mganga mkuu wa wilaya ya Geita,Dk.Noel Makuza
aliyeambatana na watalaam wengine waliovalia mavazi maalum ya kuzua
magonjwa ya kuambukiza.
Mgonjwa
huyo alifariki usiku wa kuamkia juzi kutokana na kusumbuliwa na tatizo
la Kuharisha na Kutapika damu pamoja na kutokwa na damu puani hali
ambayo ilisababisha hofu kubwa na baadhi ya wakazi wa mji wa Geita
walianza kuvumisha kuwepo kwa mgonjwa wa Ebola na kuanza kusambaza
ujumbe mfupi kwenye simu za mkononi kuchukua tahadhali.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu mganga Mfawidhi wa
Hospitali ya wilaya ya Geita,Dk.Adamu Sijaona alisema hakuna mgonjwa wa
Ebola aliyefikishwa Hospitalini hapo na kudai kwamba dalili za Ebola
zinafahamika.
“Mgonjwa
huyu ,tumekaa nae kwa siku 10 alikuwa na tatizo la Madonda ya Tumbo na
alikuwa akitokwa damu puani na ukeni lakini haijathibitishwa kama ni
ebola au la ,isipokuwa dalili za Ebola zinashabihiana na dalili za
magonjwa mengine kama Homa ya Bonde la Ufa,na mengine”alisema
Dk.Sijaona.
Alisema
Vipimo vya mgonjwa huyo vimechukuliwa kwenda kwa mganga mkuu Taifa kwa
vipimo zaidi ili kujua kama alikuwa anasumbuliwa na Ugonjwa huo wa Ebola
kutokana na Hospitali hiyo kutokuwa na vipimo vya kubaini ugonjwa huo.
Akizungumzia
suala la ndugu kuzuiliwa kuona mwili wa marehemu na mwili huo kwenda
kuzikwa na Halmashauri badala ya ndugu, Dk.Sijaona alisema”Tulifanya
hivyo kwa kuwa tulikuwa na wasiwasi kwa sababu mgonjwa huyo alihisiwa
mwenye dalili za Ugonjwa wa Ebola,lakini tulichukua ndugu wawili
wakaoenda kuona alipozikwa ndugu yao.”alisema Daktari huyo.
Hata
hivyo mmoja wa ndugu wa marehemu,Mariam Boniphace alisema mdogo wake
alianza kuugua Agosti 19,mwaka huu kwa kutapika na kuharisha kawaida
alipopimwa alionekana anasumbuliwa na Malaria lakini baada ya siku tatu
alianza kutapika na kuharisha damu na damu nyingine ilikuwa inatokea
puani na sehemu za siri.
“Tunamashaka
yawezekana kuwa ni Ebola,kwa nini madakt ari wametuzuia kuaga mwili wa
marehemu wala kumgusa?,na bado wamedai wamechukua vipimo na kuvipeleka
nchi za nje kwa uchunguzi zaidi na majibu wamesema baada ya wiki moja
yatapatikana”
Katika
hatua nyingine Dk.Sijaona amewatoa wasiwasi kwamba Geita hakuna mgonjwa
wa Ebola na badala yake amewataka wananchi kuchukua tahadhali kubwa
kuhusu ugonjwa huo wanapoona dalili kama hizo kutoa taarifa mapema ikiwa
ni pamoja na kumpeleka mgonjwa hospitalini kwa uchunguzi zaidi.
Post a Comment