Mlipuko wa Ebola wazidi kushika kasi Afrika Magharibi.
Wafanyakazi wa huduma za afya (MSF) wakiandaa eneo maalum la kuhifadhi wagonjwa wa Ebola huko Monrovia Agosti. 23, 2014.
Shirika la afya duniani WHO linasema mlipuko wa ugonjwa wa Ebola unaweza kuathiri watu wengine zaidi ya 20,000 kote Afrika magharibi wakati utakapomalizika .
Shirika hilo la Umoja wa mataifa lilitoa tathmini yake alhamisi wakati walipoanza kampeni ya dola
milioni 490 kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo ambao umeuwa watu wasiopungua 1,550.
Linasema idadi ya jumla ya kesi hizo imefika 3,000, lakini inaelezewa kuwa idadi kamili inaweza kuwa juu kwa mara mbili mpaka nne zaidi.
Maambukizo mengi zaidi yametokea Liberia , Sierra Leonne na Guinea . WHO inasema mlipuko huo unaendelea kuongezeka lakini akasema nyingi ya kesi hizo ni katika maeneo machache yenye wakazi wengi.
Mapema alhamisi wizara ya afya ya Nigeria imeripoti kesi mpya mbili za Ebola na kufikia jumla ya wagonjwa nchini humo 15.
SOURCE: SAUTI YA AMERIKA
Post a Comment