HABARI KAMILI: KUMI WAMEFARIKI DUNIA NA MAJERUHI SABA, AJALI MBAYA ILIYOTOKEA MBALIZI-MBEYA
Hivi ndivyo ambavyo Daladala hiyo ilivyojibamiza muda mchache uliopita
Eneo hili la ubavuni ndipo eneo ambalo Daladala hiyo iliingia na Kujigonga
Gari hilo aina ya Tata likiwa limepaki pembeni Muda mchache baada ya kupata ajali hiyo
Askari wa usalama wa Barabarani akiwa anatazama na kuchunguza zaidi ajali hiyo
Viti vikiwa vimeharibika baada ya ajali kutokea
Hivi ndivyo Daladala hiyo iliyokuwa ikitoka Mwanjelwa kuja Mbalizi ilivyo Haribika Baada ya ajali hiyo
Mashuhuda wakiwa wamelizunguka daladala hiyo kushuhudia kllichotokea
Hapa ndipo eneo ambapo ajali imetokea , Askari wa usalama wa barabarani wakiendelea kufuatilia ajali hiyo
Ilikuwa ni Ajali mbaya
Mashuhuda
Baadhi ya Majeruhi wakiwa wanatolewa katika Hospitali ya Ifisi kuelekea Hospitali ya Rufaa Mbeya
********
WATU kumi wakiwemo watoto
wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine saba wamejeruhiwa vibaya katika
ajali iliyohusisha magari mawili.
Ajali hiyo ilitokea jana
majira ya saa nne asubuhi ikihusisha gari ndogo ya abiria maarufu daladala
lenye namba za usajili T 237 BFB aina Toyota Hiace na gari kubwa
aina ya Fuso lenye namba za usajili T 158 CSV.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa
ajali hiyo wamesema ajali hiyo ilitokea maeneo ya Mbalizi baada ya Hiace
iliyokuwa ikitokea Mbeya mjini kuelekea Mbalizi kulivaa Fuso ilikuwa ikiingia
barabarani.
Walisema inasemekana dereva wa
Hiace gari yake ilimshinda kutokana na kutelemka mlima mkali wa Mbalizi inagawa
pia walimtupia lawama dereva wa Fuso ambaye alikuwa akiingia barabarani bila
kuchukua tahadhari.
Muuguzi Mkuu wa Hospitali
teule ya Ifisi Mbalizi, Sikitu Mbilinyi, ambako Majeruhi na marehemu
walikimbizwa hapo alithibitisha kupokea majeruhi 7 ambapo alisema kati yao ni
wanawake 3 na wanaume 4.
Alisema kati ya majeruhi hao
wawili wamepewa rufaa kwenda hospitali ya Rufaa Mbeya kutokana na kuhitaji
msaada zaidi huklu wengine wakiendelea kupatiwa msaada wa haraka ili kunusuru
hali zao.
Mbilinyi aliongeza kuwa pia
wamepokea miili ya marehemu 10 wakiwemo watoto wawili na Wanawake wanne na
Wanaume wanne.
Hata hivyo majina ya majeruhi
na marehemu hayajaweza kupatikana mara moja kutokana na kuwa katika hali mbaya
ambapo Dereva wa Fuso akitokomea mara baada ya tukio. SOURCE: Mbeya Yetu Blog.
Post a Comment