Header Ads

Shinji Kagawa njiani kuondoka Man United – hii ndio klabu anayoenda

1409307188735_wps_2_File_photo_of_Manchester_
Wakati wa utambulisho rasmi wa Angel Di Maria jana, kocha qa man United Louis Van Gaal alithibitishqa kwamba kuna kundi la wachezaji litaondoka mpaka kufikia mwishoni mwa wiki hii.
Leo hii zimetoka taarifa kwamba kiungo wa kimataifa wa Japan, Shinji Kagawa ni mmoja wa wachezaji
wanaondoka kwenye klabu hiyo kabla ya kuisha kwa dirisha la usajili.
Shinji anatarajiwa kujiunga na klabu yake ya zamani ya Borrusia Dortmund kwa ada ya uhamisho wa £8m.
Mchezaji huyo anatarajiwa kuwasili Ujerumani leo hii tayari kwa kufanyiwa vipimo vya afya ili kukamilisha usajili wake Dortmund.
Kagawa alijiunga na Man United miaka mitatu iliyopita kwa ada ya uhamisho wa £12m.

No comments

Powered by Blogger.