Header Ads

OKWI KUKABIDHIWA KWA PATRICK PHIRI ZANZIBAR LEO


OKWI LEO BAADA YA KUKABIDHIWA JEZI YA SIMBA JANA.


Emmanuel Okwi ambaye amesaini mkataba mpya wa kuichezea Simba ataungana na Wenzake Zanzibar leo Ijumaa.

Okwi ataungana na wenzake, lakini kabla ya kuingia kambini atakabidhiwa kwa Kocha Patrick Phiri.
Simba iko kambini Zanzibar na Okwi ataungana na wachezaji wengine wa Simba wakiwa chini ya Phiri, Selemani Matola na Iddi Pazi.
Phiri na Okwi wamewahi kufanya kazi pamoja kabla ya Mzambia huyo kuondoka na kurejea kwao.
Simba imemsajili Okwi ambaye hata hivyo bado ana kesi na Yanga ambayo imeshitaki kwa TFF kutokana na utovu wa nidhamu.
Akiwa Zanzibar, Okwi ataendelea na mazoezi na wenzake huku akishughulikia kesi yake na Yanga mabayo imetaka afungiwe pamoja na kulipa kitita cha dola 200,000.

No comments

Powered by Blogger.