MCHUNGAJI AFIKISHWA MAHAKAMANI, AISHI NA MKE WA MUUMINI WAKE
Pichani ni Mchungaji, Israel Mwakifuna, wa Kanisa la Jeshi la Bwana(JB)lililopo Nzovwe jijini Mbeya
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, ambapo wananchi wengi wanaamini
Mchungaji ni sehemu ya kukimbilia kueleza matatizo yao hususani migogoro ya
kindoa, hali imekuwa tofauti jijini Mbeya.
Utata umeibuka baada ya Mchungaji, Israel Mwakifuna, wa Kanisa la
Jeshi la Bwana(JB)lililopo Nzovwe jijini Mbeya amefikishwa katika Mahakama ya mwanzo
ya Iyunga jijini Mbeya akituhumiwa kuishi na mke wa mtu ambaye ni muumini wake.
Mchungaji
huyo alifikishwa juzi mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Iyunga, Nuru Lyimo
akisaidiwa na Washauri wa mahakama Edson Mbeba na Rehema Haonga.
Kesi
hiyo ya madai namba 51/2014 imepelekwa mahakamani hapo na William Daimon Mwasubila(23)mkazi wa Nzovwe
ambapo imedaiwa mahakamani Mchungaji kuishi na mke wake aitwaye Helena Mkea(21)
kwa muda wa miezi minne sasa.
Mlalamikaji katika Kesi hiyo, Mwasubila aliiambia mahakama kuwa
alikuwa akiishi na mkewe bila tatizo lakini matatizo yalianza pindi mkewe
aliposhika ujauzito na kuamua kwenda kwa wakwe zake kwa matazamio baada ya
mapishano yaliyodhaniwa kusababishwa na ujauzito hali ambayo alikubali.
Mwasubila alieendelea kuiambia mahakama kuwa mkewe alimuoa
kihalali kupitia mshenga wake aliyefahamika kwa jina la Edward Mwangoje ambapo
walifuata taratibu zote za mila kwa kulipa kiingilio cha mlangoni 50,000,kufungua
20,000,adhabu 50,000, kuku wawili, mashuka, mablanketi mawili na majembe
mawili.
Alivitaja vitu vingine alivyolipia kama mahali kuwa ni mkaja wa
mama 150,000 ambapo alilipa elfu hamsini,Mbuzi wawili jike na dume,n'gombe
watatu dume ambao kila mmoja akiwa na thamani ya shilingi 300,000 na kupokelewa
na wazazi kupitia kwa mshenga Octoba 20 mwaka 2013 eneo la Airport Jijini
Mbeya.
Alisema mgogoro katika ndoa yao ulianza baada ya Mume kuzikuta SMS
za mapenzi kwenye simu ya mkewe kwenda kwa mchungaji Mwakifuna ambapo alitoa
taarifa kwa wazazi wapande zote mbili ambapo walijadili na kuondoa tofauti hizo
na kuamua kuwasamehe.
Aliongeza kuwa muda mfupi
baada ya mazungumzo Mchungaji aliendelea kuwa na mahusiano ya kimapenzi na
muumini wake hali iliyosababisha mke wa mchungaji Mwakifuna kuondoka kwa mumewe
miezi minne iliyopita baada ya yeye(Mlalamikaji) kwenda kikazi Sumbawanga
Mkoani Rukwa ambapo mkewe alihamia kwa Mchungaji wake na kuanza kuishi kama mke
na mume.
Aliendelea kuiambia Mahakama kuwa Baada ya kutoka Sumabwanga alipata taarifa kuwa mkewe anaishi na
mchungaji ambapo aliamua kutoa taarifa Polisi kituo cha Nzovwe.
Alisema Jeshi la Polisi lilifika nyumbani kwa Mchungaji na
Kumkuta mkewe akiwa na mtoto wake wa
kike mwenye umri wa wiki moja na nusu ndipo alipokamatwa Agosti 25 na kufikishwa mahakamani Agosti 26,
mwaka huu.
source: mbeya yetu blog
Post a Comment