UKWELI KUHUSU: MTOTO ABAKWA NA KUUAWA KINYAMA HUKO SHINYANGA AZIKWA
Mazishi ya mwanafunzi aliyeuawa kikatili kwa kubakwa kisha kutobolewa macho na
watu wasiofahamika kisha mwili wake kutupwa kichakani katika kijiji cha
Nhelegani kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga yamefanyika katika
makaburi ya familia katika kijiji cha Negezi kata ya Mwawaza katika manispaa ya
Shinyanga.
Mwanafunzi huyo aliyekuwa anasoma
darasa la tatu katika shule ya Msingi Negezi iliyopo kata ya Mwawaza manispaa
ya Shinyanga alikutwa ameuawa kwa kubakwa kisha kutobolewa Agosti 25 mwaka huu
saa saba mchana katika kitongoji cha Kashampa kijiji cha Nhelegani kata ya
Kizumbi.
Akizungumza wakati wa mazishi ya mwili
wa marehemu yaliyofanyika LEO MCHANA naibu meya wa manispaa ya Shinyanga
David Nkulila alilaani kitendo cha kinyama alichofanyiwa mtoto huyo huku
akiitaka jamii kushirikiana na jeshi la polisi katika kuwafichua wahusika wa
mauaji hayo.
“Kifo cha mtoto huyu ni mapenzi ya
mungu yaliyosababishwa na wanadamu wabaya,naomba suala la hili lifuatiliwe
hatuhitaji siasa katika hili inauma sana kwani vitendo vya ukatili dhidi ya
watoto vinatishia amani Shinyanga”,alieleza Nkulila.
Kwa upande wake Intelijensia mkoa
wa Shinyanga Bundala Maige alisema suala la ulinzi kwa watoto ni jamii nzima na
kwamba wahalifu wako ndani ya jamii hivyo kuitaka jamii kuwafichua wahalifu hao
ili kukomesha vitendo vya ukatili vinavyoendelea mkoani Shinyanga.
Naye mwenyekiti wa mtaa wa Masekelo
kata ya Masekelo yalikofanyika mazishi ya mtoto huyo bwana Peter Juma Kitundu
alisema kifo cha mtoto huyo kinatia simanzi kubwa kwani kimesababishwa na
binadamu huku akiiomba serikali kulifanyia uchunguzi wa kina tukio hilo
na lisiingizwe suala la siasa.
Kwa upande wake mwinjilisti
Emmanuel Donald Kaswalala aliyeendesha ibada ya mazishi alilaani vitendo vya
kikatili wanavyofanyiwa watotot huku akiiomba jamii kumrudia mwenyezi mungu kwa
kuondokana na matendo mabaya.
Post a Comment