YANGA SASA YAMDAI OKWI ZAIDI YA DOLA 500,000, YATISHIA KWENDA FIFA
Mambo
yanazidi kupamba moto baada ya uongozi wa Yanga kusema ulipeleka jina la
mshambuliaji Emmanuel Okwi katika majina yake ya wachezaji.
Yanga
imesema ilipeleka jina hilo, hivyo inashangazwa kusikia
Simba imemsajili na imeamua kuongeza adhabu ya kutaka afungiwe na ile faini kutoka dola 200,000 iongezeke nyingine ya dola 500,000.
Simba imemsajili na imeamua kuongeza adhabu ya kutaka afungiwe na ile faini kutoka dola 200,000 iongezeke nyingine ya dola 500,000.
Kama
hiyo haitoshi, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amewaambia waandishi wa habari
leo jijini Dar kwamba walituma barua ya kutaka kuvunja mkataba kwa TFF
wakieleza nia yao.
“TFF
haikuwa bado imejibu, Okwi akatuandikia sisi barua lakini sisi hatukiandika
kwake. Ilipaswa naye apelike TFF.
“Simba
pia wamefanya kosa, wanajua Okwi bado ana mkataba na Yanga, lakini wamekurupuka
na kumsajili ambalo ni kosa kwa mujibu wa Fifa na Caf.
“Yanga
tunajua bado suala la wachezaji wa kigeni liko wazi, dirisha halijafungwa. Ndiyo
maana tulipeleka jina lake tukijua kama suala la kupunguza mchezaji mmoja
litafika, tutalifanyia kazi.
“Simba
na Okwi, wote wanapaswa kufungiwa kutokana na kukiuka vipengele hivi. Sisi tuliamini
ni watu wa busara ambao wanakuja kuendeleza soka, lakini hizi ni vurugu ambazo
hazijengi,” alisema Manji.
“Tunaamini
suala letu TFF italishughulikia ndani ya siku saba, ikishindikana tukakwenda
Caf, Fifa au Cas (mahakama ya soka).”
HAYA NDIYO INAYASISITIZA YANGA KWA OKWI:
1. Tokea lakini laki 2 hadi laki 5, Simba pia inawahusu,
wasingekubali, wangefuata utaratibu, wamemfuata mchezaji kabla ya kuanza na
timu.
2.
Wataiomba TFF, ikiwezekana Okwi afungiwe kucheza moja kwa moja,
pia Simba kwa kuwa wamemsajili akiwa bado na mkataba.
3.
Hawajavunja mkataba, barua aliyoiandikia Yanga, ilitakiwa
aindikie TFF kwa kuwa yenye haikumuandikia yeye.
4.
Wametoa siku 7 kwa TFF
kusikiliza na kutoa majibu ya kesi yao, la sivyo watalipeleka Caf, Fifa au Cas.SOURCE: SALEHE JEMBE
Post a Comment