WANAWAKE WANAVYOSABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
Kesi ya wanaume
kupungukiwa nguvu za kiume zimezidi kushika kasi, kiasi cha kufanya dawa za
kuongeza nguvu hizo kuwa maarufu na zenye mahitaji makubwa katika jamii.
Waganga wa kienyeji
wamekuwa wakitumia dawa hizo kama tiba ya msingi
ya kuwavutia wateja kwenye biashara zao. Hii inaonesha kuwa tatizo hili ni kubwa miongoni mwa wanaume wengi katika jamii yetu.
ya kuwavutia wateja kwenye biashara zao. Hii inaonesha kuwa tatizo hili ni kubwa miongoni mwa wanaume wengi katika jamii yetu.
Hata hivyo, utafiti
unaonesha kwamba wengi kati ya wanaume waliowahi kutumia dawa za asili na zile
za hospitali kuondokana na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume hawakufanikiwa
kupata tiba ya kudumu, matokeo yake wamegeuzwa kuwa watumwa wa kila wanapotaka
kushiriki tendo lazima wale dawa ya kuwasaidia kuamsha hisia zao.
Kwa wanaume,
ukosefu wa nguvu ni jambo linalouma na kuondoa kabisa ujasiri. Wengi kati yao
wako tayari kutumia pesa na uwezo wao wote kuhakikisha kuwa heshima ya tendo la
ndoa ikuwa katika miliki yao daima.
Lakini, watafiti wa
masuala ya mapenzi wamegundua kuwa wengi kati ya hao wanaolalamika kupungukiwa
nguvu za kiume, hawafahamu chanzo cha matatizo na namna wanavyoweza kuepukana
na kasoro hizo.
Ushahidi
uliopatikana kwa waathirika wa tatizo hili, unaonesha kuwa wanaume wanapokabili
upungufu wa nguvu za kiume huishia kujuta na kujilaumu wenyewe bila kutazama
upande wa pili wa washirika wao, namaanisha wanawake.
Zipo kesi za
wanaume kujiua au kujinyofoa sehemu zao za siri kwa sababu ya kushindwa katika
tendo la ndoa. Hali hii inatoa picha kwamba wanaume wengi hujitwika mzigo wa
lawama wenyewe.
Wanawake huchangia
kwa kiasi kikubwa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, jambo ambalo nasi tunalithibitisha
kwa ushahidi wa kitaalamu.
1: KAULI
Miongoni mwa mambo
ambayo mwanaume hataki kuyasikia yakitoka kwenye kinywa cha mwanamke ni
kuambiwa HAWEZI TENDO LA NDOA.
Mwanamke akimwambia
mwanaume wakati au baada ya tendo kuwa hawezi, atakuwa amemsababishia tatizo
kubwa la kisaikolojia ambalo litampelekea kupotea nguvu za kiume taratibu.
Msaada unaohitajika
kwa mwanamke anayekutana na mwanaume dhaifu kwenye tendo si kumwambia hawezi,
bali ni kumtia moyo na kumsaidia kuweza.
Wanawake
wamewasababishia waume zao upungufu wa nguvu za kiume kwa kuwaambia maneno kama
haya: “Yaani siku hizi sijui umekuwaje, yaani huwezi kazi kabisa!”
2: UJUZI
Wanawake wengi hasa
waliopo kwenye ndoa,
wanapuuza ujuzi kwenye tendo la ndoa. Hawajishughulishi
kumsaidia mwanaume ‘kuwika’, si wabunifu na watundu, jambo hili humfanya mwanaume
kushiriki tendo kwa kutegemea kupanda kwa hisia zake mwenyewe, hivyo anapokuwa
amechoka au ana mawazo, hawezi kusisimka kwa vile hapati ushirikiano toka kwa
mwenzake.
Pamoja na wengi
kutokuwa wajuzi, lakini wapo wengine ambao ni watundu mno kwenye sita kwa sita
kiasi cha kumfanya mwanaume ajione kama mgeni wa mchezo huo.
Kimtazamo, wanaume
hupenda sana ushindi wakati wa ‘kazi’, lakini pale wanapogeuzwa ‘chekechea’
hupunguza uwezo wa kujiamini na kuruhusu hofu kuongezeka mawazoni mwao, hivyo
kuwasababishia tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Inashauriwa kwamba,
mwanamke anapokuwa na uelewa mkubwa wa masuala ya mapenzi hasa wakati wa tendo,
asioneshe kiwango kikubwa kwa haraka bali amchukulie mwenzake kama mwanafunzi,
asiwe na maneno kama: “Leo nakuja kukupa vitu adimu kuliko vya juzi, hakuna
kulala kasi mtindo mmoja.” Kauli hizi huwaogopesha wanaume na kuwafanya
wapungukiwe na nguvu.
3:USAFI
Mwanamke anapokuwa si msafi, huweza kumsababishia mwanaume matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume. Sote tunafahamu umuhimu wa usafi wa mwili na kero za uchafu wakati wa tendo, hivyo ni wazi kuwa mwanamke akiwa mchafu atamfanya mwanaume apoteze msisimko na uwezo wa tendo la ndoa. Unadhifu wa mavazi na mwili ni muhimu sana katika mapenzi.

4:GUBU
Jambo lingine linaloweza kumsababishia mwanaume upungufu wa nguvu za kiume ni gubu au karaha za maneno ya uchokozi yasiyokuwa na kichwa wala miguu. Uchokonozi wa mambo, ugomvi, usaliti na hali ya kutokuwa na staha ni mambo yanayosababisha tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Mwanamke anapokuwa
mwingi wa maneno ya kashfa, dharau na matusi huweza kumfanya mume amchukie na
kutopenda kushiriki naye tendo. Uchunguzi unaonesha kwamba wanawake walioolewa
wenye tabia hii, huwafanya waume zao wawe na msisimko wa kimapenzi kwa wanawake
wa nje kuliko wake zao hao.
5:USALITI
Tabia ya usaliti kwa mwanamke ni chanzo kingine cha mwanaume kupata tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Mwanaume anapoona, kuhisi au kubaini kuwa anasalitiwa, huumia sana moyoni, maumivu ambayo hatimaye humfanya muhusika kuwa na mawazo mengi ambayo humuondolea hamu ya tendo.

Naomba nimalizie
kwa kusema somo hili limezungumzia zaidi wanawake, lakini vipengele vilivyomo
kwenye somo hili vinatumika pia kwa upande wa wanaume kuwasababishia wanawake
matatizo ya kupoteza msisimko wakati wa tendo.
Post a Comment