ACT YAWATAKA UKAWA KUTOKUTANA NA RAISI KIKWETE
Fabian,Mwananchi Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT) kimewataka wajumbe wa bunge la katiba wanaotetea katiba ya wananchi Ukawa kukataa kukutana na Raisi kwa ajili ya mazungumzo. Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya
basketi ball wilayani Bariadi Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Lukas Limbu kwa lengo la kutabulisha chama chake na sera za chama chake. Limbu alisema kuwa wajumbe wanaounda kundi la Ukawa wasikubali kukutana na raisi kwa ajili ya maridhiano kuhusu bunge la katika kuendelea na kwamba chama tawala tayari wameshatoa tamko kuwa bunge hilo liendeleena mchakato huo. “tunasikitishwa na Raisi wetu kwa nini anataka majadiliano na Ukawa wakati chama chake wameshaadhimia kuwa bunge hilo liendelee sasa anataka kuwaeleza nini ukawa nawaomba wasiende kujadiliana naye kwani yeye ameshafanya maamuzi kupitia chama chache”Alisema
Limbu. Limbu alisema kume kuwepo na kitendawili kuhusu upatikanaji wa katiba mpya, imekuwa ni tofauti na tulivyo kuwa tukitarajia watanzania wengi badala ya kupata katiba yenye maslahi na watanzania, wabunge na wajumbe walioko bungeni wapo kwa maslahi yao binafsi na maslahi ya vyama vyao badala kushughulikia kilichowapeleka kwa ajili ya watanzania. Limbu alisema kuwa wananchi walitoa maoni yao na kupendekeza kuwepo na serikali tatu lakini chama cha ccm na wajumbe wake walikaa na kujadiliana juu ya jambo hilo na kukataa mapendekezo ya wananchi hali ambayo inatia wasiwasi wa kupatikana kwa katiba mpya. Katika hatua nyingine alidai kuwa kumekuwepo na unyanyasaji juu ya watoto wenye ulemavu wa ngozi (albinism) wanaishi kama wakimbizi ndani ya nchi yao huku wakiteseka katika makambi waliyowekwa ili kunusuru matukio ya kukatwa. “tunasikitika sana kuna baadhi ya watanzania wenzetu wanaishi kama wakimbizi nadani ya nchi yao tumeona wenzetu walemavu wa ngozi wamekusanywa na kuwekwa kambini ili wasitafutwe kukatwa viungo,kwani jeshi la polisi Halipo mpaka kuwanyia uhuru wa kuishi na wazazi wao hawa watoto mpaka wawekwe kambini” Alisema Limbu. Kwa upande wake katibu wa
Ngome ya Vijana Taifa Philip Malack alisema tumeamua kuanzisha chama kwa ajili ya kupigania maslahi ya wanyonge ili kila mmoja afaidi matunda ya nchi yake. Vijana wengi tumekuwa tukitumikishwa katika vyama vya siasa hali inayopelelekea kupoteza uhalisia wa demokrasiana kutumikishwa na baadhi ya viongozi bila kufaidika na vyama na badala yake wanatutelekeza. Malack alisema ili nchi iweze kujitawala inahitaji ardhi, siasa safi, uongozi bora na watu kupata mahitaji ambayo yanamwezesha kila mtanzania kufaidika na matunda ya nchi yake Aidha ACT waliweza kufungua ofisi ya Mkoa mjini Bariadi, tawi la ACT kidinda na walijiopatia wanachama 287 waliofika kuchukua kadi za chama hicho huku wakiahidi watakiunga mkono katika harakati zake za kuongoza nchi. MWISHO
Post a Comment