UKWELI KUHUSU: Polisi amgonga mtoto, Atoroka na kutelekeza gari
Polisi mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja, aliyekuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kasi, Jumapili iliyopita alimgonga mtoto wa kike, Zahara
Almeda katika barabara ya Mji Mpya mkoani Morogoro.
Katika tukio ambalo mwandishi wa habari hizi alilishuhudia, mara tu
baada ya kumgonga mtoto aliyekuwa akitoka sokoni kununua magimbi na
mihogo, askari huyo aliteremka na kukimbia akiliacha nyuma gari lake
lililokuwa bado halijazimwa, ambalo ndani yake kulikuwa na kofia yake.
Wananchi waliojawa na hasira baada ya tukio hilo walilizingira gari
hilo na kutaka kulichoma moto, lakini busara za baadhi yao ziliwezesha
kitendo hicho kutofanyika na baadaye trafiki alifika kudili na tatizo
hilo
Mmoja wa watu walioshuhudia ajali hiyo iliyolihusu gari aina ya
Toyota Baloon lenye namba za usajili T 5** AUE, alisema mtoto
aliyegongwa alikuwa akitokea sokoni Mji Mpya, akiwa amebeba kikapu
kichwani.
Mtu huyo aliyejitambulisha kwa jina la Sudi Kiwamba, alisema binti
huyo alikuwa ameshavuka barabara, lakini wakati akijiandaa kuvuka msingi
wa pembeni gari hilo lilimfuata katika jitihada za kumkwepa mwendesha
pikipiki.
Hata hivyo, siku moja baada ya tukio hilo, mwandishi wetu alizungumza
na baba mzazi wa mtoto huyo alisema mwanaye anaendelea vizuri na mtu
aliyemgonga alikwenda hospitalini kumjulia hali kwani aliamini alikuwa
amefariki.
Post a Comment