Header Ads

KIPENZI CHAMCHANA MDOMO NGASSA AKIPAMBANA Z



Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa, amelazimika kutofanya mazoezi na timu yake baada kuchanika mdomo kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya KMKM ya Zanzibar ambapo Yanga ilishinda kwa mabao 2-0.

Yanga inayojitayarisha na msimu mpya, inatarajia kucheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa ili kujiweka sawa kabla ya kuwavaa Azam FC katika mechi ya Ngao ya Jamii.
Kocha wa Yanga, Marcio Maximo, amesema kuwa mchezaji huyo aliumia wakati wa mchezo huo ambapo alipigwa na kiwiko cha mchezaji wa KMKM na ndiyo sababu hakuwepo kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyoanza jana.
Ngassa hakufanya mazoezi na timu yake katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola ila alifika na kukaa jukwani na kushuhudia wachezaji wenzake wakiendelea na mazoezi chini ya Maximo.
“Ngasa ameumia mdomo ila anaendelea vizuri na anaweza kucheza michezo ya kirafiki inayokuja,” alisema Maximo.

No comments

Powered by Blogger.