Header Ads

UKWELI KUHUSU: MFANYABIASHARA AFIA GESTI ARUSHA




Arusha. 
Mfanyabiashara maarufu jijini Arusha, Olais Metili mkazi wa Uzunguni jijini hapa, amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni ya Hoteli Diamond Motel iliyopo eneo la Sakina jijini hapa.

Mwili wa mfanyabishara huyo anayemiliki mali mbalimbali ikiwamo mgahawa wa Bite Bite na duka maarufu la vinyago eneo la Kisongo uligundulika jana saa 7:00 mchana, wakati wahudumu wa hoteli hiyo wakitaka kufanya usafi chumba alichokuwa amepanga.

Mfanyabiashara huyo mwenye umri unaokadiriwa kufikia miaka 56 , ilidaiwa aliingia hotelini hapo na mwanamke mmoja ambaye hata hivyo, haikujulikana muda ambao alitoka.

“ Metili (Marehemu) alifika katika hoteli hiyo akiwa ameongozana na mwanamke mmoja ambaye hajafahamika na kuingia katika chumba chake na haijulikani aliondoka muda gani huyo mwanamke,” alisema mmoja wa wahudumu wa hoteli hiyo.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas hakupatikana jana kuelezea taarifa za awali za uchunguzi wa kifo hicho, lakini maofisa wa polisi waliuchukua mwili huo, wakisema huenda kesho taarifa itatolewa rasmi.

Tukio hili, linakumbusha kifo cha Kada wa CCM, Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya UVCCM Taifa, Benson Mollel ambaye alifariki dunia katika hoteli ya Lash Garden eneo la Jakaranda ambapo pia alidaiwa aliingia katika chumba hicho na mwanamke.

Matukio ya kufa katika nyumba za wageni, katika jiji la Arusha, yanahusisha na matumizi ya pombe kali au dawa za nguvu za kiume kwa wanaume wengi ambapo dawa zimekuwa zikiuzwa katika maeneo mengi jijini hapa bila ya udhibiti mkali

No comments

Powered by Blogger.