KISA CHA KUTISHA CHA DADA HUYU NA SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA
Msichana anayetambulika kwa jina moja la Mary (23) anayedai kuchoshwa na kazi ya kubebeshwa madawa ya kulevya.
Msichana aliyejitambulisha
kwa jina moja la Mary (23), mkazi wa Dar ambaye ni mwenyeji wa Nyegezi,
Mwanza, ameangua kilio na kusema; ‘nabebeshwa madawa ya kulevya (unga),
nalipwa kiduchu hadi nimechoka’.Awali,
gazeti hili lilitonywa na vyanzo vyake juu ya kuwepo kwa ishu hiyo
maeneo ya Manzese, Dar ambapo uchunguzi ulifanyika na kumnasa binti huyo
ambaye alifunguka kila kitu.
Akizungumza na
wanahabari wetu kwa uoga mkubwa, Mary alidai kwamba alichukuliwa kutoka
kijijini kwao huko Nyegezi ambapo alipofikishwa Dar, alijikuta
akiunganishwa kwenye mtandao wa kuuza ‘unga’.
“Nililetwa Dar mwaka jana na mwanaume mmoja, aliniahidi kunitafutia
kazi, niliishi naye kama mtoto wake.“Zilipita kama wiki mbili tangu
aliponileta bila kuniambia
nitafanya kazi gani, siku moja ndipo akanipeleka Mitaa ya Magomeni
(Dar) na kuniambia nitakuwa nafanya shughuli za kuuza unga huku nikiishi nyumbani kwake na yeye ndiye bosi wangu.
“Nilishangaa sana kuona ile ndiyo kazi niliyoahidiwa kuja kuifanya
Dar. Nilianza kumlilia bosi wangu anirudishe kwetu Mwanza lakini
alinigomea, hata pale nilipotafuta
kisingizio cha kumwambia nimemkumbuka mama yangu, aliniambia nimtumie
nauli aje Dar,” alisema binti huyo akilengwalengwa na machozi.
Baadhi ya madawa ya kulevya yaliyowahi kunaswa.
Aliendelea kusimulia kwa majonzi kwamba, siku hadi siku amekuwa akiiona dunia ikimuelemea kwa kuwa amechoka na hayupo radhi kufanya shughuli hiyo, kwani mbali na hatari yake haoni manufaa anayopata.
Alisema, awali alikuwa akilipwa Sh. 3,000 kila siku kwa kupakia
kwenye paketi na alipobadilishiwa kitengo na kuanza kuhesabu kete na
kubebeshwa amekuwa akilipwa kiduchu, yaani Sh. 50,000 kwa mwezi.
“Hii kazi sitaki hata kuisikia, nimeshafanya kwa mwaka mmoja sasa, sijapata faida yoyote kwani nalipwa kiduchu huku nikiishi kwa hofu muda wote hivyo nimechoka.“Kuna
kipindi mama yangu alikuja na kufikia kwake, alimnyanyasa na kumnyima
nauli ya kurudi Mwanza. Alikuwa ananiambia kama vipi nikajiuze nipate
nauli ya mama yangu.
Kamanda Godfrey Nzowa.
“Sikuwa tayari kufanya hivyo, mama yangu akasaidiwa na jirani akasafirishwa kurudi kijijini Mwanza,” alisema na kuongeza:
“Kuna wakati
ananitishia maisha endapo nitatoa siri popote, jambo ambalo limenifanya
nikose uhuru na amani ya maisha, ndiyo maana nimeshukuru kukutana na
magazeti ya Global Publishers nitue huu mzigo.”
Katika kile kinachozidi kumtia hofu ni pale alipoambiwa siku chache
zijazo ataanza kusafirisha unga nchi mbalimbali na kupata utajiri mnono
jambo ambalo hataki kulisikia, kwa kuwa anaogopa kuozea jela hivyo
kikubwa anachohitaji ni msaada wa nauli ya kurudi kwao Mwanza akamsaidie
mama yake ambaye ni mzee na ni mgonjwa.
Post a Comment