KAGERA WACHUKUA TAHADHARI DHIDI YA EBOLA
Mkuu
wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Massawe akitoa ufafanuzi namna
Serikali livyojipanga kukabiliana na ugonjwa wa Ebola mkoani humo kwa
kuongeza vifaa kinga na kuwawezesha kielimu wataalam wa afya wanaofanya
kazi ya uchunguzi wa dalili za ugonjwa huo walioko katika vituo vya
ukaguzi mpakani.
Afisa
Afya wa Kituo cha ukaguzi cha Kabanga, mpakani mwa Tanzania na Burundi
Bw. Amos Mangaluke akipitia fomu zilizojazwa na raia kutoka nje ya nchi
wanaotumia mpaka huo kufuatia zoezi la uchunguzi wa dalili za awali
za ugonjwa wa Ebola linalofanyika kituoni hapo.
Ofisi ya Uhamiaji ya Kabanga mpakani mwa Tanzania na Burundi.
Kizuizi cha magari katika mpaka wa Kabanga unaotenganisha Tanzania na Burundi, Wilayani Ngara.
Na. Aron Msigwa –MAELEZO,Kagera.
Mkoa
wa Kagera umechukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Ebola kwa kuongeza
nguvu katika udhibiti na ukaguzi wa raia wa kigeni kutoka nchi za
Burundi, Rwanda, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanaoingia
nchini Tanzania kupitia vituo vya mpakani vya mkoa huo.
Akizungumza
katika mahojiano maalum wilayani Ngara, Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali
mstaafu Fabian Massawe amesema kuwa kufuatia hali hiyo serikali kupitia
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeongeza vifaa kinga na kuwawezesha
kielimu wataalam wa afya walioko katika hospitali za mkoa huo na vituo
vya ukaguzi mpakani.
Amesema
kuwa mkoa huo kijiografia unapakana na nchi tatu zikiwemo Uganda kwa
upande wa Kaskazini, Rwanda na Burundi kwa upande wa magharibi na
kuongeza kuwa mkoa kupitia kamati za Afya na wataalam wa afya walioko
maeneo yote ya vituo vya ukaguzi wanafanya kazi zao ipasavyo kwa
kuhakikisha kuwa kila anayeingia nchini kupitia vituo hivyo anachunguzwa
dalili za Ebola.
“Mkoa
wa Kagera kama tunavyojua unapakana kwa karibu sana na nchi za Burundi,
Rwanda na Uganda, kuna mwingiliano mkubwa sana wa watu kutoka eneo moja
kwenda jingine hapa lazima tuchukue tahadhari kubwa , ninawahakikishia
wananchi kuwa tumejipanga vizuri katika kuimarisha uchunguzi kupitia
kamati zetu za afya” Amesisitiza.
Amesema
kufuatia uwepo wa ugonjwa huo katika nchi ya jirani ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo, uongozi wa mkoa kupitia kamati ya Afya na ile ya
Ulinzi na Usalama unaendelea kuwaelimisha wananchi kupitia vituo vya
mbalimbali vya radio vya mkoa huo kuhusu dalili za ugonjwa huo , namna
ya kujikinga na namna ya kutoa taarifa kwa mamlaka husika endapo
watabaini mtu mwenye dalili za ugonjwa huo.
Kwa
upande wake Afisa Afya wa Kituo cha ukaguzi cha Kabanga, mpakani mwa
Tanzania na Burundi Bw. Amos Mangaluke akizungumzia hali ya ukaguzi wa
raia wanaoingia nchini kupitia mpaka huo amesema kuwa zoezi la uchunguzi
wa dalili za awali za ugonjwa wa Ebola linafanyika kwa ufanisi mkubwa
kufuatia kituo chake kuwa na vifaa kinga vinavyomsaidia wakati wa
utekelezaji wa majukumu yake.
Amesema
takribani watu 500 wanaotumia mpaka huo wa Kabanga huchunguzwa afya zao
kwa siku ambapo hujaza fomu maalum ya taarifa ambayo hutumiwa na
wataalam wa afya kituoni hapo.
Post a Comment