Header Ads

MADAKTARI WANASWA LIVE WAKIMTOA MIMBA MWANAFUNZI SHUHUDIA


Madaktari wawili, Hamis Chacha (kushoto) na Shengena wanaotuhumiwa kwa jaribio la utoaji mimba.
 

IMEBUMA kwao! Madaktari wawili, Hamis Chacha na Shengena wa zahanati moja iliyopo Yombo Buza jijini Dar wamejikuta katika wakati mgumu baada ya polisi kuwaibukia na kuwaweka chini ya ulinzi kwa madai ya  kufanya jaribio la kumchoropoa mimba msichana mmoja aliyedaiwa kuwa ni denti wa chuo f’lani cha digrii za juu, Dar.

Tukio hilo la aina yake lilijiri Agostii 25, mwaka huu katika zahanati hiyo ambayo jina tunalihifadhi kwa sasa.Awali, Operesheni Fichua Maovu  ‘OFM’ ya Global Publishers  ikiwa katika pitapita zake ilinasa tukio hilo ambapo polisi walikuwa ndani ya zahanati hiyo wakiwaweka chini ya ulinzi madaktari hao.
OFM ilifanikiwa kuzama ndani ya zahanati hiyo na kuingia kwenye chumba cha kilichodaiwa hutumika katika zoezi hilo.
 
Vifaa vilivyokusudiwa kutumiwa na madakta hao katika zoezi la utoaji wa mimba.
 
Daktari Shengena alipoona kamera ya OFM alitaka kukimbia licha ya kuwepo kwa askari ndani ambapo walitumia nguvu za ziada kuwadhibiti vyema na kuingizwa ndani ya chumba alichokuwemo mwenzake ambaye naye alinaswa akiwa na vifaa vilivyodaiwa ni vya kuchomolea mimba akiwa amevificha kwenye mfuko wa rambo.
 
Madaktari wakiwa chini ya ulinzi wa makamanda wa OFM.
 
Baada ya maafande kuwaweka chini ya ulinzi, madaktari hao walizua kituko kufuatia kuzitupa chini shilingi 40,000 walizopewa na denti huyo kama malipo ya kazi hiyo wakidhani ni za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ‘Takukuru’.
 
kiasi cha fedha cha Shillingi arobaini elfu walicholipwa madaktari kwa ajili ya kufanikisha zoezi la utoji mimba.
 
Wakizungumza na waandishi wetu baada ya kuulizwa nini kilikuwa kikiendelea chumbani humo, Dokta Chacha alidai kuwa mgonjwa huyo ana tatizo kwenye kizazi hivyo alikuwa akitaka kusafishwa na si kutoa mimba maelezo yalikosolewa na denti huyo aliyedai kuwa alikwendwa kwa mapatano ya kumchoma mimba ili akaendelee na masomo chuoni.
 
Binti (denti) aliyekusudiwa kutolewa mimba.
 Akijibu kuhusu kwa nini alivificha vifaa va kutolea mimba kwenye mfuko, Dokta Chacha alijiumauma na kusema denti huyo alifuata taratibu zote kama wagonjwa wengine, lakini alishindwa kuonesha risiti au cheti cha kumsajili mgonjwa huyo kwa ajili ya matibabu.
 
Zahanati iliyotumiwa na madaktari hao katika jaribio la utoaji mimba.
 Kichekesho kingine kilikuwa wakati OFM na wanausalama wakitoka nje ya zahanati hiyo na watuhumiwa na kukuta kwenye maeneo mengine kukiwa kweupe na kusemekana kuwa, madaktari na manesi walioshuhudia wenzao wakitaitiwa walitoka nduki kwa kuogopa ushahidi.

Mwishowe watuhumiwa hao walifikishwa katika Kituo cha Kidogo cha Polisi Buza na kufunguliwa jalada lenye Kumbukumbu Na. BUZ/RB/32/2014 kabla ya baadaye kufikishwa Kituo cha Polisi Chang’ombe, Dar kwa ajili ya mahojiano ya kina kuhusiana na sakata hilo.

No comments

Powered by Blogger.