Familia yajiua Iringa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi.
Kilolo. Mwanamke mmoja wa
Kijiji cha Mtitu wilayani hapa, Grace Lubava (33), amemuua mtoto wake
kwa sumu na kisha naye kujiua kwa njia hiyohiyo na baadaye mumewe,
George King’ung’e (45), kujinyonga kwa kamba kutokana na vifo hivyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi
alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi na kwamba mama huyo
alifariki dunia alipokuwa akipatiwa matibabu katika Zahanati ya Kilolo.
“Kifo cha mama na mtoto kilitokea baada ya mumewe
kumzuia mkewe kwenda kumwona baba yake ambaye alikuwa amelazwa katika
Hospitali ya Tosamaganga,” alisema Mungi.
Alisema kuwa mume alimzuia mke huyo kwenda
hospitali kwa madai kuwa alikuwa anakwenda kwenye mambo yake binafsi
jambo ambalo lilimkera mwanamke huyo kiasi cha kufikia uamuzi huo.
Kamanda Mungi alisema baada ya King’ung’e kubaini vifo hivyo na msingi wake, aliamua kwenda porini na kujinyonga.

source:Mwananchi
Post a Comment