WALINZI WA JADI SUNGUSUNGU WILAYANI KAHAMA WAJIPANGA KUMALIZA TATIZO LA MAUAJI YA VIKONGWE.

WALINZI
wa Jadi "Sungusungu "wilayani Kahama,mkoani Shinyanga wameweka mkakati
wa kuhakikisha wanakabiliana na wauaji wa Vikongwe kwa imani za
Kishirikina ambao katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Shinyanga ni tatizo kubwa.
Katibu Mkuu wa
Sungusungu wilaya ya Kahama,Zephania Lupambe ameyasema hayo jana kwenye
maadhimisho mapya ya siku ya Sungusungu yaliyofanyika kwenye Kata ya
Chona na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.
Hata
hivyo Lupambe amesema katika kukabiliana na hali hiyo kuna changamoto
nyingi ambazo ni pamoja na walinzi hao wa jadi kuwa wahusika wakubwa wa
mauaji hayo,hali ambayo inachangia waharifu hao kufichwa.
Amesema
katika matukio hayo baadhi ya walinzi hao wa jadi wamekuwa wakibainika
kujihusisha na mauaji hayo,hali ambayo amewataka kuacha mara moja tabia
hiyo,kwani mkakati uliopo sasa likitokea tukio la kikongwe kuuawa
kuanzia kitongoji husika wanaanza kuwajibishwa.
Kwa
upande wake Mbunge wa Jimbo la Kahama,James Lembeli ameuunga mkono
mpango wa sungusungu hao wa kukomesha mauaji hayo na kuwataka
wakishawakamata wasijichukulie sheria mkononi ya kuwauwa na badala yake
wawapeleke kwenye vyombo vya sheria.
Lembeli amesema mpango ni mzuri iwapo utatekelezwa kama ulivyopangwa kwakuwa wauaji wenyewe wanawafahamu na wana ishi nao hivyo ni rahisi kuwajua kuliko hata polisi hivyo aliwaunga mkono kwa kuwachangia Shilingi Milioni Mbili,zitakazosaidia kuimarisha mkakati huo.
Post a Comment