ROBIN VAN PERSIE KAMILI GADO KUPIGA MZIGO DHIDI YA SUNDERLAND
Amerudi: Robin van Persie amerudi mazoezini na alifurahia kukuatana na nahodha wa United, Wayne Rooney.
MANCHESTER United itamtumia mshambuliaji
wake, Mholanzi, Robin van Persie katika mchezo wa jumapili wa ligi kuu
soka England dhidi ya Sunderland.
Wakati huu mkurugenzi mkuu wa United ,
Ed Woodward akiwa na mipango ya kuleta wachezaji wawili kabla ya
kufungwa kwa dirisha la usajili, ameendelea kufuatilia namna anavyoweza
kumsajili Angel di Maria.
Pia anaangalia mwenendo wa Sami Khedira katika klabu hiyo ya Real Madrd.
Wakati huo huo kocha wa United, Louis
van Gaal alitoa habari njema jana alhamisi baada ya Van Persie kurudi
mazoezini kwa mara ya kwanza.
Van Persie hajawahi kucheza chini ya
kocha mpya wa Man United katika klabu hiyo tangu kumalizika kwa fainali
za kombe la dunia nchini Brazil majira ya kiangazi mwaka huu.
Kocha Van Gaal aliiongoza Uholanzi
kutwaa nafasi ya tatu na Van Perise ndiye alikuwa nahodha wake, na baada
ya fainali hizo alimpa mapumziko ili kukusanya nguvu mpya.
Mholanzi alifanya mazoezi United ikijiandaa kuchuana na Sunderland katika mchezo wa pili wa ligi kuu England.
Jembe jipya: Van Persie amerudi kazini
wakati huu United ikihitaji ushindi kwa nguvu zote baada ya kupoteza
mechi ya kwanza kwa mabao 2-1 katika uwanja wake wa Old Trafford
jumamosi iliyopita dhidi ya Swansea.
Post a Comment