Header Ads

MUUNGWANA NI VITENDO: KWA WEWE MSANII INAKUHUSU

 MUUNGWANA NI VITENDO.

Pichani ni aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwa anazungumza na Mfalme wa Muziki wa Pop Duniani na Mwanamuziki Mashuhuri wa Marekani, Marehemu Michael Joseph Jackson Ikulu Jijini Dar es salaam.

Picha hii ilipigwa Mwaka 1992 wakati Mfalme huyu wa muziki wa Pop wa Marekani, hayati Michael Jackson alipoitembelea Tanzania na kufanya Kitendo cha Kiungwana kwa kufika katika Shule Maalum ya Watoto Yatima na wenye Mtindio wa Ubongo iliyopo Sinza, Jijini Dar es salaam.

Mwanamuziki huyo aliyekuwa maarufu zaidi duniani hadi anakufa 2009, alifika nchini akiwa Balozi wa ziara ya Umoja wa Mataifa na akapokelewa kiserikali na Waziri wa Mambo ya Nje wakati huo, hayati Balozi Ahmed Hassan Diria.

Michael Jackson alitua jioni moja Uwanja wa Ndege wa Dar akiwa amevalia shati la kijani lenye mikono mirefu, suruali nyeusi na kofia nyeusi, akapandishwa kwenye Gari Maalum iliyompeleka hadi Kilimanjaro Hotel (wakati huo) ambayo baadaye ikawa Kilimanjaro Hotel Kempinsk, na sasa ikiitwa Hyatt Regency Dar es Salaam.

Mashabiki waliokuwa na habari walijazana uwanja wa ndege Dar “kumkodolea mimacho” mwanamuziki huyo wakati huo akiwa na umri mdogo tu wa miaka 34, mbali na wale waliomfuata hadi kwenye hoteli hiyo. Wakaungana na wale waliokuwa wakimsubiri hapo kumshangilia kwa mbinja na mayowe ya furaha.

Pia, mashabiki waliokuwa na habari za ujio na ratiba yake, walijitokeza kwa wingi na kumshangaa vilivyo, The Wacko Jacko alipotembelea shule hiyo ya Sinza, kesho yake.

Katika ziara yake hiyo ya siku mbili nchini, alikutana na mkuu wa nchi ambaye wakati huo alikuwa Rais Ali Hassan Mwinyi.

Hivyo Ndivyo Michael Joseph Jackson alivyofika Tanzania na kushikana mikono na watoto wa Sinza miaka karibu 20 iliyopita!.

Picha hii ni sehemu ya Kampeni Maalum ya Ukurasa wa "Watanzania Mashuhuri" ya Kuwafariji na kuhamasisha Msaada na Fursa kwa Watoto Yatima na wale wenye Mtindio wa Ubongo hapa Nchini, Shime Watanzania kila mmoja kwa Nafasi yake tushikamane kwenye hili. Uungwana ni Vitendo.

Picha ni kwa Hisani kubwa ya Idara ya Habari Maelezo

Pichani ni aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwa anazungumza na aliyekuwa Mfalme wa Muziki wa Pop Duniani na Mwanamuziki Mashuhuri wa Marekani, Marehemu Michael Joseph Jackson Ikulu Jijini Dar es salaam.

      Picha hii ilipigwa Mwaka 1992 wakati Mfalme huyu wa muziki wa Pop wa Marekani, hayati Michael Jackson alipoitembelea Tanzania na kufanya Kitendo cha Kiungwana kwa kufika katika Shule Maalum ya Watoto Yatima na wenye Mtindio wa Ubongo iliyopo Sinza, Jijini Dar es salaam.
Mwanamuziki huyo aliyekuwa maarufu zaidi duniani hadi anakufa 2009, alifika nchini akiwa Balozi wa ziara ya Umoja wa Mataifa na akapokelewa kiserikali na Waziri wa Mambo ya Nje wakati huo, hayati Balozi Ahmed Hassan Diria.
      Michael Jackson alitua jioni moja Uwanja wa Ndege wa Dar akiwa amevalia shati la kijani lenye mikono mirefu, suruali nyeusi na kofia nyeusi, akapandishwa kwenye Gari Maalum iliyompeleka hadi Kilimanjaro Hotel (wakati huo) ambayo baadaye ikawa Kilimanjaro Hotel Kempinsk, na sasa ikiitwa Hyatt Regency Dar es Salaam.
    Mashabiki waliokuwa na habari walijazana uwanja wa ndege Dar “kumkodolea mimacho” mwanamuziki huyo wakati huo akiwa na umri mdogo tu wa miaka 34, mbali na wale waliomfuata hadi kwenye hoteli hiyo. Wakaungana na wale waliokuwa wakimsubiri hapo kumshangilia kwa mbinja na mayowe ya furaha.
Pia, mashabiki waliokuwa na habari za ujio na ratiba yake, walijitokeza kwa wingi na kumshangaa vilivyo, The Wacko Jacko alipotembelea shule hiyo ya Sinza, kesho yake.
Katika ziara yake hiyo ya siku mbili nchini, alikutana na mkuu wa nchi ambaye wakati huo alikuwa Rais Ali Hassan Mwinyi.
      Hivyo Ndivyo Michael Joseph Jackson alivyofika Tanzania na kushikana mikono na watoto wa Sinza miaka karibu 20 iliyopita!.
     Picha hii ni sehemu ya Kampeni Maalum ya Ukurasa wa "Watanzania Mashuhuri" ya Kuwafariji na kuhamasisha Msaada na Fursa kwa Watoto Yatima na wale wenye Mtindio wa Ubongo hapa Nchini, Shime Watanzania kila mmoja kwa Nafasi yake tushikamane kwenye hili. Uungwana ni Vitendo.

SOURCE: S.U.A

No comments

Powered by Blogger.