Header Ads

BARCELONA TAYARI KUMSAJILI BEKI WA KUSHAMBULIA TOKA BRAZIL




Beki la kushambulia: Beki huyo amefunga mabao sita katika mechi 124 alizoichezea Sao Paulo miaka mitatu iliyopita
 
KLABU ya Barcelona imekubali kumsajili beki wa kulia Douglas Pereira kutoka Sao Paulo kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 3.19, vigogo hao wa Katalumya wamethibitisha jana.
Uhamisho unaweza kupanda kwa Pauni Milioni 1.2 zaidi kwa ajili ya beki huyo mwenye umri wa miaka 24 kulingana idadi ya mechi atakazocheza katika klabu yake mpya.
Pereira atajiunga na klabu hiyo ya La Liga kwa mkataba wa miaka mitano iwapo atafaulu vipimo vya afya wiki hii nchini Hispania.

No comments

Powered by Blogger.