Header Ads

VIJANA CUF KUANDAMANA KESHO LICHA YA ONYO LA POLISI

CHAMA cha Wananchi CUF kupitia Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Wananchi (JUVICUF), kime[panga kufanya maandamano makubwa Februari 13, 2015 kuanzia Bugururuni Rosana hadi Ofisi za Tume ya taifa ya Uchaguzi na baade Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa JUVICUF, Hamidu Bobali amesema maandamano hayo yamenyimwa kibali na jeshi la Polisi lakini kwakuwa walisha jiandaa kuyafanya wao watayafanya ili kufikisha ujumbe wao .

“Tumeandaa manaandamano ya amani kwa lengo la kuitaka tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),kuongeza siku za kuandikisha wapiga kura kutoka saba (7) zilizo pangwa sasa hadi 14 na kulaani ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na polisi,” alisema Bobali.

Bobali Februari 9,mwaka huu waliliandikia jeshi la polisi barua ya kuwataarifu juu ya kufanyika kwa maandamano hayo ya amani na waliainisha maudhui ya maandamano hayo na kuwa ni kuitaka NEC,kuongeza siku za kuandikisha wapiga kura kutoka siku saba hadi 14, na kulaani ukiukwaji wa haki za binadamu waliodai unafanywa na jeshi hilo.

Aidha, Majibu ya barua hiyo yaliyotolewa leo na jeshi hilo, yamesitisha maandamano hayo kwa madai kuwa njia hiyo haiwezi kuleta suluhu la madai yao.

Maandamano hayo yamepamngwa kuanzia saa nne asubuhi.

Hata hivyo, Kufuatia sakata hilo, Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akizungumza na vyombo vya habari ofisi kwake ametangaza kupiga
marufuku maandamano hayo kwa kile alichoeleza kuwa yana leongo la kuvunja amani.

Kamishna Kova amesema Jeshi la Polisi watatumia uwezo wao kwa misingi ya sheria ili kudhibiti
maandamano hayo ambayo hayana nia nzuri.

“Maandamano yao hayana mantiki yoyote, tuliwaita viongozi wao ambao ni Maulid Said Naibu Katibu
na Masoud Said Masoud ili waongozane na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu kwenda NEC
kupata ufumbuzi wa maoni yao,” alisema Kova.

Source; Father Kidevu

No comments

Powered by Blogger.