Header Ads

BARCELONA AIZIMA MAN CITY 2 -1 ETIHAD

MANCHESTER City imesogea karibu na mlango wa kutokea katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, kufuatia kipigo cha mabao 2-1 nyumbani usiku
huu Uwanja wa Etihad kutoka kwa Barcelona katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 Bora.

Hata hivyo ilionekana Mbaya wa City usiku huu alikuwa mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Luis Suarez aliyeifungia Barcelona mabao yote hayo.

Suarez, mfungaji bora wa zamani England alfunga bao la kwanza dakika ya 16 akiwa ndani
ya boksi, kabla ya kuongeza la pili dakika ya 30 akimalizia kazi nzuri ya Lionel Messi.

Sergio Aguero aliifungia Manchester City bao la kufutia machozi zikiwa zimbeki dakika 21. City
ilimpoteza Gael Clichy aliyeonyeshwa kadi ya
pili ya njano na Messi akakosa penalti dakika ya mwisho.

Kikosi cha Manchester City kilikuwa; Hart, Zabaleta, Kompany, Demichelis, Clichy, Nasri/
Fernandinho dk61, Milner, Fernando, Silva/ Sagna dk78, Dzeko/Bony dk68 na Aguero.

Aidha kikosi cha Barcelona: Ter Stegen, Alves/Adriano dk75,
Pique, Mascherano, Jordi Alba, Rakitic/Mathieu dk71, Busquets, Iniesta, Messi, Suarez na
Neymar/Pedro dk80.

No comments

Powered by Blogger.