Misri Yaishambulia ISIS Libya
Mkuu wa kanisa la Coptic Taarifa kutoka Misri zasema kuwa, ndege za kijeshi zimewashambulia
wapiganaji wa jihadi nchini Libya kwa mabomu, baada ya kutolewa kwa mkanda wa video ulioonyesha wakristo wa Misri wa madhehebu ya
Coptic wakikatwa shingo.
Jeshi la Misri linasema kuwa limelenga kambi za Islamic State, kituo cha mafunzo na maghala ya
silaha, katika shambulizi hilo la mapema leo alfajiri.
Walioshuhudia wanasema kuwa, mji wa Derna ulioko mashariki mwa Libya na ambao umetekwa
na wapiganaji wa jihadi ndio ulioshambuliwa vibaya.
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi, amesema kuwa mashambulio hayo ya angani ni jibu kwa wapiganaji hao ambao walitoa mikanda hiyo ya video hapo jana jumapili ili onyesha waumini kumi kati ya 21 waliotekwa nyara wakichinjwa.
Jeshi la Misri limetoa taarifa kwa vyombo vya habari inayosema kuwa raia wa taifa hilo walioko mbali ama karibu, wanafaa kuelewa kuwa wana
jeshi la taifa linalowalinda kokote waliko. Taarifa kutoka Misri zasema kuwa, ndege za kijeshi zimewashambulia wapiganaji wa jihadi Nchini Libya kwa mabomu, baada ya kutolewa kwa mkanda wa video ulioonyesha wakristo wa Misri
wa madhehebu ya Coptic wakikatwa shingo.
Jeshi la Misri linasema kuwa limelenga kambi za Islamic State, kituo cha mafunzo na maghala ya
silaha, katika shambulizi hilo la mapema leo alfajiri.
Walioshuhudia wanasema kuwa, mji wa Derna ulioko mashariki mwa Libya na ambao umetekwa na wapiganaji wa jihadi ndio ulioshambuliwa vibaya.
Post a Comment