Header Ads

MAMBO MAKUBWA 10 YATAKAYO HARIBU MAISHA YAKO

1. Kujiweka wa mwisho na Kujinyima muda wa kufurahi /kustarehe.
Maisha yako yamejengwa kwa vipande vidogo vidogo ambavyo kila kimoja kina nafasi yake,
na kikikosekana, basi vingine havitakaa kwenye nafasi zake na kuharibu maisha yote.
Wengi tumekuwa tunawapa nafasi wengine kwanza na kuamua kujiweka sisi wa mwisho.
Matokeo yake, unajinyima muda wa
kupumzika, kula, kustarehe nk! Matokeo yake
huwi na furaha na maisha yako!

2.Kukubali kuendeshwa na matukio mabaya yanayopita.
Kuhisi kwa kuwa kuna kitu Fulani kibaya kilikutokea kwenye maisha yako basi maishahayatawezekana tena. Pengine ulifiwa, kufukuzwa kazi, shule, kuibiwa au kufilisika.

3.Kukubali kuzungukwa na watu wasiokufaa.
Ni rahisi, Siku zote watu waliokubali
kushindwa, huwa na sababu za kukupa kwa nini wameshindwa kimaisha, na ukikaa karibu
nao watakupa sababu hizi na kukufanya uamini kwamba huu ndio ukweli, na hutakuwa
tayari kupiga hatua zaidi.

4.Kukimbia matatizo na kuogopa kushindwa.
Je wajua? Ukikimbia matatizo yako, siku zote yatakimbia pamoja nawe. Usikimbie tatizo, likabili na kuamka haraka kila tunapoanguka.
Na epuka Kuhisi kuna mtu mwingine
anahusika na furaha yako.

5. Kuharibu Maisha ya Mwingine ili Ufanikiwe.
Ukiharibu maisha ya mwingine, unaharibu ya kwako! Unaweza kuita Karma, Gundu, au majina mengine, lakini jua ya kwamba hii
hutokea kweli. Pia ni ngumu kukaa na hayo mafanikio Maana hutakuwa na plani ya pili ya mafanikio zaidi ya kudhurumu, kuiba, kuua nk!

6. Kuamini Wewe ni Mifupa na nyama tu!
Hili ni kosa kubwa sana maishani, wengi huamini binadamu n mifupa na nyama tu, hivyo hakuna hata ya kufanya kazi kwa bidii
kwa kuwa tu “eti” Mwisho wa siku tutakufa na kuzikwa! Je, Unawaachia nini wanao na kizazi
chako? Je kwa nini hasa Mungu alitupa utashi tofauti na Mbuzi na wanyama wengine? Kumbuka, Tungeamua kuamini kuwa sisi ni
Nyama na mifupa tu, kusingekuwa na Magari, Simu, Majengo ya kisasa, na Hata hii dini tuliyonayo tusingeipata. “do your part, make world a better place”

7.Kulaumu Vitu vinavyotokea na kutokuwa tayari kutafuta suluhisho. Pengine kwa kutotaka kufanya maamuzi magumu au kutojua
Majukumu yako ni yapi (badilika)

8. Kuamini kila kinachosemwa naWataalamu
Siku hizi kila sekta kuna watu wanaojiita wataalamu (mimi mmoja wapo!) Lakini nasikitika kukuambia kuwa, wengi wa wataalamu hawa, hawako sahihi kwani siku
hizi watu wanapata kipato kutokana na kuyaelewa matatizo ya watu na si kujua suluhisho.
Usimuamini mtu eti tu kwa kuwa analielezea kwa uzuri na analielewa tatizo lako bali muamini anayeweza kutoa suluhisho linalokuwa msaada kwa tatizo lako

9. Kuhisi huwezi kwa kuwa kuna mtu anakuambia hivyo.
Kuna watu maishani wapo sii tu kwa
kukukwamisha wewe, bali pia kumkwamisha kila anayewazunguka. Ukiona hakubaliki kwa jinsi ulivyo, basi jua huko mahali sahihi. Usikubali kuishi kama mtu mwingine kwa kuwa tu unataka kukubalika maishani.

10. Kuona huhitaji chochote cha kusoma
Maisha yanachekesha! Kitu kinaweza kuwepo leo, na kesho kisikuwepo. Kama kuna kitu unataka kufanya, fanya sasahivi. Kama ni wazo la muda mrefu, basi anza leo kutekeleza kidogo kidogo. Kila muda una changamoto zake. Hata tajiri mkubwa duniani Bill gates anachangamoto zake kulingana na nafasi aliyonayo.

Source; Mr. Clever

No comments

Powered by Blogger.