Header Ads

JK amkaribisha Rais wa Ujerumani Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais wa Ujerumani Joachim Gauck yuko nchini Tanzania kwa ziara rasmi ya siku sita, Kiongozi huyo amepokewa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania.

Rais Gauck ambae anatarajiwa kufanya mazungumzo na matabaka mbalimbali ya viongozi nchini Tanzania amewasili jana
jioni.

Aidha, Baada ya hafla ya mapokezi
iliyofanyika katika Ikulu ya Dar es Salaam viongozi hao wawili, Rais Kikwete na Gauck, walifanya mazungumzo ya faragha, na baadae kukutana na waandshi
habari.

Hata hivyo, Pembezoni mwa mazungumzo ya viongozi hao wawili, kulifanyika pia mazungumzo ya wake wa marais, Mama Salma Kikwete na Bibi, Daniela Schadt, mke wa rais
Gauck.

Naye, Mke huyo wa Rais Gauck
atazitembelea taasisi tatu, ikiwemo
WAMA, inayosimamiwa na rais mke wa Rais Kikwete na kisha hospitali ya tiba maalum za viungo ya CCBRT ya jijini Dar es Salaam.

No comments

Powered by Blogger.