Header Ads

FAHAMU DALILI 8 ZA MWANAMKE ANAETOKA NJE YA NDOA


Wataalamu wa maswala ya mahusiano wanaamini
kwamba, mwanamke anapotoka nje ya ndoa yake, inakuwa rahisi sana kubainika au kufumaniwa
kuliko ilivyo kwa mwanaume.

Hii inatokana na ukweli kwamba, hisia zinakuwa na nafasi kubwa sana kwa mwanamke, kwani
mwanamke huishi kwa hisia zaidi kuliko mwanaume.

Bado nasisitiza kwamba, haipaswi na siyo sahihi mtu kuchukulia dalili hizi kama ushahidi wa mpenzi wake kutoka nje ya ndoa, Uchunguzi wa kina kufuatia dalili hizi ni muhimu
sana.

Zifuatazo hapa chini ni baadhi ya dalili zinazoweza kuonyeshwa na mwanamke ambaye anatoka au yupo kwenye harakati za kutoka nje ya ndoa yake;-

1. KUCHELEWA: Kuna wakati mwanamke anaweza
kuaga kwamba anakwenda saluni au kusuka,
badala ya kurejea kwa muda ambao umezoeleka,
anachukua muda mrefu hata mara tatu zaidi. kuna
wakati kwenda sokoni huchukua saa kadhaa bila
kujali soko liko umbali gani. Kama ni mara moja
sawa, lakini ikishakuwa zaidi ya mara moja
huenda kuna tatizo la kukosa uaminifu.

2. KUBADILI MAENEO: Hebu chukulia kwamba,
mwanamke amezoea kwenda soko fulani la
karibu, hospitali fulani ya karibu, saluni fulani ya
karibu na hata nyumba fulani ya ibada ya karibu.
Unapoona anahama maeneo ya karibu ya huduma
na kwenda ya mbali, bila sababu ya msingi, huna
budi kuanza kutuhumu mwenendo mbaya.
Siyo lazima kuhama kokote kuwe na mwenendo
mbaya, lakini kama kuhama kwenyewe kunatia
shaka kwa sababu maelezo ya kuhama huko
hayana msingi, mwanaume ana kila sababu ya
kuchunguza kama hakuna usaliti unao anywa.

3. UNUNUZI USIO WA KAWAIDA: Kama
mwanamke anatoka nje ya ndoa yake kwa ajili ya
kupata fedha, basi atakuwa na mabadiliko
makubwa katika mtindo wake wa manunuzi.
Atakuwa ananunua vitu vya thamani kubwa kuliko
uwezo wake, atakuwa na fedha nyingi tofauti na
ambazo angekuwa nazo na pengine kumiliki mali
kama nyumba kwa siri.

4. KUANZISHA VURUGU: Kuna wakati mwanamke
anayetoka nje ya ndoa huanzisha vurugu za
makusudi na mumewe. Lengo la kuanzisha
vurugu hizo ni ili apate nafasi ya kujifanya
amezira na kuondoka nyumbani kwa muda.
Huo muda anapoondoka nyumbani kujifanya
kakerwa na vurugu hizo ndiyo muda ambao
anautumia kwenda kwa hawara yake.

5. KUSITISHA UAMINIFU: Mwanamke anayetoka
nje ya ndoa, mara nyingi husimamisha
kumwamini mumewe, yaani hayuko tayari
kushiriki masuala ya siri, ambayo wanandoa huwa
wanashiriki.
Husita kumshirikisha mumewe kwenye mambo
yake mengi. Lakini pia husita kumuomba
mumewe ushauri, kama alivyokuwa akifanya siku
za nyuma.

6. KUACHA KUVAA PETE: Kuna sababu nyingi ni
kwa nini mwanamke anaweza kuacha kuvaa pete
yake ya ndoa. Moja ya sababu hizo ni kusalitiwa
na mumewe au ndoa yake kuwa kwenye
misukosuko mikubwa sana.
Lakini nje ya misukosuko mikubwa ya ndoa,
sababu nyingine inayoweza kumpelekea
mwanamke kuvua mara kwa mara au moja kwa
moja pete yake ya ndoa, ni kuwa na uhusiano nje
ya ndoa yake.

7. KUONESHA WASIWASI: Kama mwanamke
anatoka nje ya ndoa yake , ni lazima atakuwa na
wasiwasi na mashaka yasiyo na sababu mbele ya
mume wake.
Anaweza kuonesha kutotulia kwa aina fulani kana
kwamba, anahofia kuna siri itatoka au kuna kitu
ambacho tayari mume wake anakijua dhidi yake.
Mara nyingi wasiwasi na mashaka humtawala
sana mwanamke anayetoka nje , hasa katika hatua
zake za awali za kutoka nje.

8. KUZUNGUMZIA KUACHWA: Kuna wakati
mwanamke anaweza kuwa anatoa kauli za
kuonesha kwamba, kama mwanaume anaona
vipi , wanaweza kuachana.
Kama kila penye ugomvi kidogo tu mwanamke
anakimbilia kusema, “kama ni kuachana, tuachane
tu” hiyo inaweza kuwa ni dalili mbaya kwa
mwanamke anayetoka nje ya ndoa kwa sababu
hana tena upendo na mumewe

No comments

Powered by Blogger.