Header Ads

Ndege za Kivita za Shambulia Ngome ya Boko haram

Ndege za kivita za Nigeria jana zilizishambulia kambi za mafunzo, maficho ya silaha na magari ya wanamgambo wa kundi la Boko Haram katika msitu wa kaskazini mashariki wa Samibisa.

Msemaji wa jeshi la Nigeria Meja Jenerali Chris Olukolade amesema kuwa wanamgambo wengi wa kundi la Boko Haram waliuliwa kwenye mashambulizi hayo huku wengine wakikimbilia katika maeneo mbalimbali ya msitu na nje ya kambi zao za mafunzo baada ya mashambulizi.

Baada ya kupita mwaka mmoja ambapo wanamgambo wa Boko Haram wameonekana kusonga mbele huku wakiteka maeneo mengi, kuua maelfu ya watu na kuwateka nyara mamia ya watu wengi na wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto hali ya mambo inaonekana kuwageukia baada ya nchi kadhaa ambazo ziko jirani na Nigeria kuamua kuanzisha mashambulizi dhidi ya kundi hilo.

No comments

Powered by Blogger.