Header Ads

TANGA HALI TETE

Hali ya wasiwasi imeendelea kutanda miongoni mwa wananchi huku askari wakiendelea
kumiminika kwenda katika mapango ya Amboni yaliyopo nje kidogo na Jiji la Tanga kukabiliana na wahalifu wanaodaiwa kujificha kwenye mapango
hayo.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa majira ya saa 5:00 asubuhi magari kadhaa yakiwamo ya kubebea wagonjwa (ambulance) yalionekana yakielekea kwenye mapango hayo.

Mmoja wa wakazi wa kitongoji cha Karasha ambaye ni mtumishi mstaafu wa serikali ambaye
aliomba jina lake lisitajwe, alisema kutokana na operesheni inayofanywa na vikosi hivyo tangu juzi, inadaiwa kuwa wahalifu wamekimbilia katika msitu
wa Mbogo ambao upo kilometa chache kutoka mapango ya Amboni.

Wahalifu hao wamekuwa wakihisiwa na baadhi ya wananchi kuwa huenda ni magaidi.

Wakati hayo yakiendelea, wazungumzaji wakuu wa
mamlaka za Serikali wamekuwa na usiri mkubwa wa kutoa maelezo kuhusiana na tukio hilo kama
kuna watuhumiwa waliokamatwa.

Bofya hapa kusoma zaidi: NIPASHE

No comments

Powered by Blogger.