Header Ads

Je unajua ni hatari kumdadisi mpenzi wako alitembea na wangapi?


KATIKA mapenzi kuna mambo ambayo hayastahili kupewa muda wa kuyajadili. Hii ni kutokana na
ukweli kwamba, mengine yanaweza kutibua furaha iliyopo na kuweza kupindisha maisha yenu.

Kwa kuthibitisha hilo, sikia kisa hiki. Jamaa mmoja aliyefahamika kwa jina la Rashid alibahatika kumpata mke mzuri sana aliyefahamika kwa jina la Wahida. Yaani
mwanamke ambaye kila mwanaume akimuona ni
lazima atamani kuwa naye.

Baada ya mwanaume huyo kumuoa, waliishi kwa
muda mrefu sana na ndoa yao ilikuwa ikitawaliwa
na furaha siku zote. Wakabahatika kupata watoto
wawili. Hakika mwanamke huyo alikuwa mke kwa
maana halisi ya mke.

Alikuwa akimheshimu sana mumewe na kumpatia
kila aina ya furaha. Kwa kifupi ilikuwa ni ndoa ya
kuigwa. Siku moja Rashid alikutana na rafiki yake
wa muda mrefu sana.

Mazungumzo yao yalikuwa mengi lakini ikafika
mahali yule rafiki akamuuliza Rashid kama
ameshaoa. Rashid akajibu kuwa kamuoa
msichana mmoja anayeitwa Wahida. Yule jamaa
akashangaa kusikia Rashid kamuoa Wahida,
mwanamke ambaye siku za nyuma alikuwa ni
changudoa.

Rashid aliposikia kuwa Wahida alikuwa
changudoa, ati akaumia sana na akaanza visa kwa
mkewe na hatimaye wakaachana. Akaoa
msichana mwingine dogodogo kutoka kijijini
ambaye hajaguswa. Alichokiona kwenye ndoa
yake hiyo ya pili alijuta hadi akamkumbuka
Wahida.

Tunajifunza nini kwenye kisa hiki? Ni kwamba,
unapokutana na mpenzi wako kwa mara ya
kwanza kuna mambo ya msingi ambayo kiukweli
unastahili kuyajua. Hapa namaanisha historia ya
maisha yake. Unapotaka kujua historia ya maisha
ya mpenzi wako siyo lazima kila kitu ujue.
Mengine yaache abaki nayo kwani hata
akikuambia hayawezi kukusaidia kiviiile.

Lipo hili swali la umeshwahi kutembea na
wanaume/wanawake wangapi hadi leo? Hili si zuri
kumuuliza mpenzi wako
Nina sababu mbili. Kwanza ni vigumu sana kupata
jibu la kweli, yaani tarajia kudanganywa. Hapo
unaweza hata kuambiwa hajawahi kuwa na
mpenzi kumbe katika ukweli tangu ameyajua
mapenzi, ametoka nao zaidi ya kumi.

Sababu nyingine ya kwa nini hustahili kuuliza
swali hilo ni kwamba, inaweza kukufanya ukabadili
mawazo yako na hata uhusiano wenu ukakomea
hapo. Unaweza kukutana na msichana mzuri sana
mwenye kila sifa nzuri na katika historia yake ya
mapenzi anaweza kuwa ameshapita kwa wanaume
kibao kiasi kwamba hata idadi amesahau.

Sasa kama utamuuliza na yeye akawa mkweli kwako kwa kukujibu kuwa, ni wengi kiasi kwamba
hata idadi hakumbuki, utajisikiaje?

Hakika unaweza kujikuta unanyong’onyea na
kushangaa hata ile hamu ya kuendelea kuwa naye
inaisha licha ya kwamba hukustahili kuwa hivyo.

Matokeo yake unaweza kumkosa mtu ambaye
alistahili kuwa na wewe na mkaishi maisha ya
raha mustarehe.

Kuwa na idadi kubwa ni tatizo?

Kuna mtaalam mmoja aliwahi kusema kuwa,
katika maisha ya sasa hakuna mwanamke
anayeolewa akiwa na usichana wake na kama
wapo ni wachache sana. Akaeleza kuwa,
msichana akishatolewa usichana wake hata akiwa
ametembea na wanaume ishirini hana tofauti na
yule aliyetembea na wawili tu.

Mtaalam huyo akasema, tena inawezekana
aliyetembea na wengi akatulia kwenye ndoa yake
kuliko yule aliyetembea na mmoja au hajaguswa
kabisa. Hapo ndipo inapoonekana kwamba, kuwa
na historia ya kwamba uliwahi kutoka kimapenzi
na wanaume/wanawake wengi, hakuna madhara
makubwa katika ndoa.

Ndiyo maana inashauriwa kulifutilia mbali swali la
kutaka kujua idadi ya wapenzi aliyowahi kuwa nao
huyo mpenzi wako au hata kuwajua kwa majina.

Hii ni kwa sababu hata ukijua haitakusaidia
chochote zaidi ya kukuchanganya na kukufanya
ukose imani kwa mpenzi wako.

No comments

Powered by Blogger.