Ivory Coast yapaa viwango vya FIFA
Ivory Coast imepanda katika viwango vya soka Fifa baada ya kushinda Kombe la Mataifa ya
Afrika.
Equatorial Guinea, wenyeji wa Kombe la Afrika lililomalizika Jumapili, walishika nafasi ya 50
kwa mara ya kwanza.
Ivory Caost wamepanda kwa nafasi nane hadi nafasi ya 20 japokuwa Algeria bado inaendelea kuwa timu nambari moja Afrika kwa kushika
nafasi 18.
Tembo hao kwa sasa wako nafasi ya pili Afrika nyuma ya Mbweha wa Jangwani (Algeria), timu walioifunga robo fainali.
Washindi wa pili Ghana wamepanda kwa nafasi 12 na kuwa wa 25.
VIWANGO VYA FIFA 2015
KUMI BORA AFRIKA
1. Algeria
2. Ivory Coast
3. Ghana
4. Tunisia
5. Cape Verde
6. Senegal
7. Nigeria
8. Guinea
9. Cameroon
10. Congo DR
KUMI BORA DUNIANI
1. Germany
2. Argentina
3. Colombia
4. Belgium
5. Netherlands
6. Brazil
7. Portugal
8. France
9. Uruguay
10. Spain
Post a Comment