Header Ads

Lady Jaydee - Gadner alitongoza na kuwashika makalio wanawake mbele yangu


Msanii wa bongo fleva Lady Jaydee amewapa nafasi mashabiki wake kumuuliza maswali naye kuyajibu kupitia akaunti yake ya Instagram.

Ameulizwa maswali mengi, na miongoni mwa maswali hayo ni la
kuhusu ndoa yake na mtangazaji wa Radio E-FM Gadner G. Habash.

Haya ni maswali na majibu kama alivyopost Instagram.

Tunasikia umeachana na mume ni kweli au uzushi?
JIBU : Hatuja achana niliamua kumuacha

Kwanini umeachana/umemuacha mume?
JIBU : Nimemuacha kutokana na kuwa Ndoa inatakiwa iwe na maelewano, furaha, amani na
upendo. .. ila kwa bahati mbaya vyote hivyo havikuwepo , sikuwa tayari kuendelea kuishi kwa
maumivu huku niki pretend ili kuiridhisha jamii.

Huoni kama umejishushia heshma kuachana na mume?
JIBU : Sioni hivyo, ila naona nilikuwa najishushia heshma zaidi kuishi na mume asie na heshma, anaeweza kutongoza na kushika
wanawake makalio wakati mi niko jukwaani naimba.
Kuwapa mademu magari yangu waendeshe na kuyagonga wakati niko safarini . Ukiachilia mbali
vipigo. Kutembea na wahudumu wa restaurant yangu. Ushahidi ninao. …..niliwahi mkuta anawashika
mapaja na akakiri kosa bado kupigana na kuwatusi wateja pia. Kifupi ilikuwa ni ndoa ya mateso.

Baada ya kuachana unategemea kuolewa tena?
JIBU : Ni mapema kujihakikishia uolewaji mwingine, ila haimaanishi kuwa sitopenda tena. Nahitaji kuwa makini zaidi Kuchagua mtu sahihi wa kumpa moyo wangu.

Kwanini usirudiane na mumeo?
JIBU : Siwezi kurudi nyuma tena, huwa nina misimamo thabiti. Mpk kuamua kuondoka na uvumilivu nilionao mjue ni maji ya shingo. …
When i say never, I mean Never.

Uliwezaje kuishi na mume mlevi namna ile?
JIBU : Nilidhani angebadikika, so nilikuwa natoa nafasi. Iliposhindikana nikaona isiwe tabu, kila mtu na aubebe mzigo wake. Ukizingatia ananizidi umri miaka mingi, alitakiwa yeye anielekeze zaidi kuliko mimi kumuelekeza maisha mtu mzima.

Uliwezaje kuondoka?
JIBU : Nilipoamua kuwa na iwe basi, Nilitoka bila kubeba kitu. Nikasafiri kwenda USA, nikakaa huko mwezi mzima ku refresh na kujipima kama kweli ntaweza ku move on?
Niliporudi Tanzania sikukanyaga tena nyumbani, mpaka muda huu nnapo type na ku post haya majibu. Kwa ki fupi ni kuwa nili ondoka bila kuaga, sikuona sababu ya kuaga. Asanteni jamani, nafikiri nimejibu yote.

Bofya hapa kusoma zaidi; http://instagram.com/p/zCuQzCEL0j/

No comments

Powered by Blogger.