Fedha Zakwamisha kukamilika Mradi wa Mabasi yaendayo kasi DART
Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART) unakabiliwa na changamoto ya kifedha
katika ujenzi wa miundombinu, kutokana na ongezeko la mahitaji ya fedha za kuukamilisha.
Bunge lilielezwa kwamba ongezeko la mahitaji ya fedha za kukamilisha mradi huo ni Sh bilioni 64.7, ambazo kati yake Sh bilioni 20.6 ni ongezeko la mishahara na Sh bilioni 44.1 ni
ongezeko la kazi na madai mengine.
Hata hivyo, Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa, Dk Athuman Mfutakamba
alisema hayo jana wakati akiwasilisha taarifa ya
mwaka ya kamati kuanzia Januari 2014 hadi
2015.
Kamati hiyo imeishauri serikali kufanya jitihada za makusudi, kuhakikisha mradi unaendelea
kutekelezwa kama ilivyopangwa na fedha yote inayohitajika kukamilisha hatua mbalimbali za mradi, zinatengwa na kupelekwa hatua zikamilike kwa wakati.
Aidha, Kwa mujibu wa Mfutakamba, inadaiwa ongezeko
hilo limefanya mkandarasi kutoonesha utayari wa
kuanza kazi katika barabara ya Msimbazi kwa
hofu ya kutokuwepo kwa fedha za kumlipa.
Pia, Changamoto nyingine ambayo wabunge walielezwa kwamba inakabili mradi, ni uharibifu
wa miundombinu ambao baadhi ya wananchi na wafanyabiashara ndogo huvamia maeneo ya
ujenzi yanayoendelea.
Vile vile kumekuwapo tabia ya wizi wa samani za barabara, mifuniko ya maji ya mvua, maji taka na
huduma nyingine.
Source; Mpekuzi
Post a Comment