NAIBU WAZIRI WA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA, AKAGUA MRADI WA UMWAGILIAJI KAREMA
Naibu
Waziri wa Kilimo Godfrey Zambe na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rutengwe
Mwenye shati la Kitenge akimwongoza Naibu waziri kukagua
Mradi wa
Umwagiliaji Karema.
Afisa
Umwagiliaji Halmashauri ya Mpanda Yusuph Mkandi alieye nyosha mkono
akimwonesha Naibu waziri eneo litakalopitia mfereji unaojengwa kwa ajili
ya mradi wa Umwagiliaji Karema
Na Kibada Kibada –Katavi
Imelezwa
kuwa Miradi mingi ya umwangiliaji katika maeneo mengi hapa nchini
inakabiliwa na changamoto ya kutokamilika kwa wakati hali ambayo
inaongeza gharama ya ukamilishaji wake.
Hayo
yameelezwa na Naibu waziri wa Kilimo na chakula na Ushirika Godfrey
Zambe wakati akikagua mradi wa umwagiliaji wa Karema ulioko Kata ya
Karema Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi katika moja ya
ziara yake aliyoifanya kukagua na kuhimiza shughuli za maendeleo hasa
miradi ya umwagiliaji mkoani humo.
Amesema
miradi mingi ya umwagiliaji hapa nchini imefanya vibaya kutokana na
kutokamilka kwa wakati,na kuongeza kuwa hii inatokana na kuanzishwa kwa
miradi mingi ya umwagiliaji bila kukamilika kama ilivyokusudiwa na
serikali.
Amesema
Miradi hiyo ilianzishwa bila kufahamu fedha yake ya ukamilishaji
inatoka wapi,kutokana na hali hiyo seriakali imeamua kukamilisha miradi
hiyo iliyoanzishwa nyuma kuliko kuanzisha mioradi mingine mipya wakati
hii iliyopo bado kukamilika.
Amesema
nia ya kukamilisha miradi hiyo ni kutaka serikali kuanzia mwakani
angalau asilimia 25 ya chakula nchini iwe inatokane na kilimo cha
uzalishaji.
Kilimo
cha umwagiliaji kitasaidia kuondokana na tatizo la chakula hapa kuliko
kutegemea uzalishaji wa chakula kwa kutegemea mvua za msimu ambazo
haziaminiki,lakini kama uzalishaji utatumia kilimo cha umwagiliaji
kutakuwa nauhakika wa chakula cha kutosha.
Awali
Mkuuwa Mkoa wa KataviDkt Rajabu Rutengwe amemweleza naibu wazir wa
Kilimo chakula na ushirika Godfrey Zambe kuwa katika mkoa wake kuna
miradi saba ya umwagiliaji laki miradi yote hiyo bado haijakamilka tangu
kuanzishwa kwake.
Hivyo
ipo haja ya kuangalia upya hata wakandarasi wanaopatiwa kazi hizo kama
kweli uwezo wa nao wa kuweza kukamilisha miradi hiyo kwa wakati
vinghinevyo tutaendelea kupteza fedha za serikali kwa kuwa wakandarasi
wanaopewa kazi hizo hawana uwezo wa kukamilisha kazi kwa wakati hali
inayofanya mradi kuongezeka gharama kwa kukaa muda mrefu bila
kukamilika.
Mkuu huyo wa Mkoa akaeleza kuwa mirdi ya umwagiliaji katika Mkoa
Imejaa
mapungufu makubwa kwa pande zote akaomba uangaliwe utaratibu wa kupitia
miradi hiyo kuona ni wapi mapungufu hayo yalijitokeza.
Akaeleza
kuwa hata kwenye kitengo cha umwagiliaji kanda lipo tatizo kubwa kwa
kuwa wakandarasi wanapokuwa wakiendelea na kazi kunajitokeza kazi za
zianda ambazo hazikuwepo kwenye mkataba kama kazi zikijitokeza nani
anawajibika kugharamia kama siyo wizi unaofanywa na baadhi ya watu wache
ili kukwamisha miradi.
Akaomba
uangaliwe utaratibu wa kuwapatia wakandarasi kazi wenye sifa kuliko
kuwapatia miradi wakandarasi ambao hawana uwezo wa kuweza kukamilisha
miradi hiyo badala yake wataendelea kufanya kazi hizo kwa muda mrefu na
gharama kuendelea kuongezeka kila kukicha hali hiyo inaitia hasara
serikali hata miradi yenye inajengwa chini ya kiwango.
Katika Mkoa wa Katavi miradi yote ya umwagiliaji iliyoanza mwaka
2009/2010 hadi sasa hakuna mradi hata mmoja ambao umekamilika na fedha
ya serikali imewekezwa hapo.
Kwa
upande mwingine Naibu Waziri waKilimo,Chakula na Ushirika amemwagiza
Mshauri wa Kilimo wa Mkoa kuhakikisha mradi wa umwagiliaji Karema
unasimamiwa na kukamilika ili uweze kuleta tija kwa kuanza uzalishaji.
Post a Comment