Header Ads

WAMTIMUA MTAANI BAADA YA KUDAIWA KUTISHIA KUMUUA MKEWE - KAHAMA

Wananchi wa Kitongoji cha Sofi Kata ya Mhongolo wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamezingira nyumba ya Juma Madata (41) na kukusanya vitu vyake vyote ili ahame Kitongoji hicho kwa kile walichodai wamechoshwa na matendo yake mabaya ikiwemo ya kumtishia kumuua mke wake.

Tukio hilo lilitokea juzi asubuhi ambapo wananchi hao walifikia maamuzi hayo baada ya mtuhumiwa , kudaiwa kumpiga mzee wa kimila Charles Nangale baada ya kumtuhumu kuwa anania mbaya na mke wake kutokana na mke wake kuwa anakimbilia kwa mzee huyo pindi kunapotokea ugomvi wa kifamilia.

Mmoja wa wananchi John Masalu
alisema mtuhumiwa huyo amekuwa na tabia ya kumpiga mke wake mara kwa mara pindi amanapokunywa pombe huku akimtishia kumchinja mke wake na watu wengine wanaoingililia uongomvi huo.

Alisema mbali na tuhuma hiyo, mwaka jana aliwahi kuichoma moto nyumba yake kabla ya wananchi kuwahi kuzima moto uliokuwa umeanza kuteketeza baadhi ya vitu, huku akifanya vituko vingi ambavyo ni kinyume na maadili ya jamii.

Naye Ester Samweli alisema hatua hiyo ya kumtoa katika kitongoji hicho walifikia kutokana na kuhofia kuwa huenda mambo anayoyasema ya kuua mtu akayatimiza na hivyo jamii inayomzunguka kuingia katika kesi zisizokuwa za lazima.

“Sisi wanawake tunaogopa sana waume zetu kulala nje ya familia zao au kukimbia familia kama yatakuja kutokea mambo mengine, wazee walishamuonya sana pamoja na kumpiga faini lakini amekuwa akirudia makosa yaleyale tangu ahamia hapa mwaka 2010.”alisema Mama huyo.

Kwa upande wake Mtuhumiwa Juma
Madata alikana tuhuma hizo na kusema yeye ndiye aliyepigwa na mwenyekiti wa kimila, huku akishangaa wananchi kuvamia nyumba yake na kuanza kutoa vitu vyake na kwamba amekubali kuhama na familia yake ambapo alikuwa anaishi na Baba mzazi wake, mke na watoto wawili.

Naye Baba mzazi wa Mtuhumiwa, Giligili Madinda alisema “ni kweli kijana wangu amekuwa akiwasumbua wananchi wa kitongoji hicho na kumtishia mke wake kumuua licha ya kuwa namsihi aache, na mimi kwa sasa nitaishi kwa kaka yangu, na jambo walilolifanya wananchi ni zuri sana.

Pia, Mke wa Mtuhumiwa aitwaye Regina Kulwa (30) aliomba serikali iwatenganishe na mume wake kutokana na kuchoshwa na ugomvi wa kila siku pamoja na kuhofia maisha yeke.

Aidha, Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Mhongolo Ali Manyama alisema alipigiwa simu saa moja asubuhi kwamba wananchi wanataka kumuua bwana Madata ndipo walipofika eneo la tukio na kufanikiwa kumpeleka katika ofisi za Kata kwa usalama wake.

Hata hivyo, alisema watamfikisha katika kituo cha polisi kwa hatua zingine za kisheria baada ya kukamilika kumhoji katika hatua za awali ngazi ya Mtaa, huku akiwataka wananchi kuendelea kushirikiana na serikali.

Source; Kijukuu blog

2 comments:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Thanx Mabula Mussa, naona umuhimu mkubwa wa COMMUNITY BASED ORGANISATIONS (CBOs) - wananchi wengi mkoani Shinyanga hawakupata elimu stahiki na Exposure ya mambo. NAAMINI KATIKA KUELIMISHA JAMII JUU YA MAHUSIANO NA HAKI ZA BINAADAMU PAMOJA NA UTAWALA WA SHERIA. SIAMINI KAMA HIYO NJIA YA KUMFUKUZA MTAANI NI SAHIHI MAANA WAMEVUNJA NDOA YAKE NA FAMILIA ITAYUMBA - SIITOFAUTISHI NA ADHABU YA WANANCHI KUCHOMA MOTO MWIZI AU KUPIGA PANGA VIKONGWE KWA IMANI ZA UCHAWI(AMESIKILIZWA MAHAKAMA IPI HADI HIYO HUKUMU IKATOKA?). TUJIKITE KATIKA KUELIMISHA ZAIDI NA HILI NI JUKUMU LA SERIKALI NA WADAU WA MAENDELEO. JAMII YETU BADO SANA NA TUMEACHWA NYUMA SANA - HAYA NI MATOKEO NA PENGINE YAPO MAKUBWA ZAIDI. "GOD BLESS KAHAMA - THE GOLD CITY."

    ReplyDelete

Powered by Blogger.