Header Ads

Nigeria Kupewa Msaada Kupambana na Boko Haram

Waasi wa Nigeria wa kundi la Boko Haram waliushambulia mji wa Monguno katika jimbo la Borno na kuiteka kambi ya kijeshi iliyoko
katika mji huo huku waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry akiahidi nchi yake itaipa serikali ya Nigeria msaada zaidi ili kukabiliana na waasi hao.

Boko Haram iliudhibiti mji wa Monguno hapo jana baada ya waziri mkuu wa uingereza john Kerry kufanya ziara nchini humo kwa mazungumzo na viongozi wa Nigeria.

Hata hivyo, Jeshi la Nigeria lilifanikiwa kuwadhibiti waasi hao kuiteka miji ya Maiduguri na Kondunga na inasemekana zaidi ya waasi 200 waliuawa katika mapambano hayo.

Aidha, Kerry amewataka wagombea wakuu wa urais nchini Nigeria kujizuia dhidi ya kuchochea ghasia baada ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa
kufanyika tarehe 14 mwezi ujao na kulaani mashambulizi ya kinyama yanayofanywa na kundi la Boko Haram.


No comments

Powered by Blogger.