Header Ads

Professor Jay: Nikki Mbishi Usiweka Silaha Chini

Msanii mkongwe wa Hip Hop Joseph Haule maarufu kama Professor Jay, ameungana na Chidi Benz kumtaka Nikki Mbishi kuachana na uamuzi aliouchukua wa kuachana na muziki akidai kuwa haulipi.

Proffesor Jay ameiambia Bongo5 leo kuwa Nikki ni msanii muhimu ambaye hatakiwi kukosekana kwenye kizazi hiki cha Hip Hop.

“Mimi nina uhakika kabisa Nikki Mbishi jinsi alivyokuwa muhimu katika game hii ya Hip Hop, alivyokuwa muhimu
katika kizazi hiki cha Hip Hop na
ninaamini alikuwa ana kila dalili za
kurithi mikoba yetu kutokana na uwezo wake mkubwa sana na ameweza kukua
na sisi toka anakuwa na muziki wake,” amesema.
“Ameanza kuona Kwanza Unity,
amewaona wakati anakua, yeye
anazungumza kila siku amewaona
akina Sugu walivyokuwa wana
struggle, amewaona akina Proffesor
Jay mpaka sasa hivi ananiita babu siku hizi haniiti dady tena kwa sababu ni moja kati ya watu wanaonieshimu,”

“Naamini amejifunza vitu vingi sana
kwa struggle ambazo tumezifanya
Kitu ambacho ninaweza nikamshauri Nikki ni kwamba hatakiwi kuweka silaha zake chini kwenye haya mapambano sababu ndo kwanzavdalili za mafanikio na maendeleo ya muziki wa Hip Hop yameanza kuonekana kwa hali ya juu". Alisema Profesa Jay

Hata hivyo, aliongeza kusema kuwa kwenye matamasha umeona wasanii wa Hip Hop tunafunika
kuliko wasanii wakuimbaimba, ingawa kuna mentality ya kuwalipa sana hela nyingi wasanii wa kuimba kuliko wasanii wa Hip Hop hali inayokatisha tamaa.

“Wasanii wengi wa Hip Hop wameingia kwenye stress na kutumia madawa ya kulevya kwa kukata tamaa ya maisha
na wanaamua kwenda vijijini kulima
tena, Kwahiyo solution sio kulikwepa
hili tatizo ni kuangalia tatizo jinsi gani unaweza ukakabiliana nalo na sio kuacha muziki ni kuangalia wapi tulikosea ukizingatia huu ni mwaka mpya 2015 mwaka uliojaa matumaini, huenda tukafanikiwa zaidi.”

No comments

Powered by Blogger.