Header Ads

BOCCO ATIMKIA ALGERIA

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ yuko mjini Ain Fakroun, Algeria kwa ajili ya mipango ya
kujiunga na klabu ya Chabab Riadhi Baladiyat, maarufu kama CRB.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, Bocco yuko huko kwa siku kadhaa baada ya kwenda mwanzoni mwa wiki kufanya mipango ya kujiunga na timu inayovalia jezi za rangi nyeusi na nyeupe.

"Timu hiyo ya Daraja la Kwanza Algeria, maarufu kama Professionnelle 2 inataka kuninunua moja kwa moja, lakini ilitaka kuniona kwanza", Alisema Bocco.

Awali, Bocco alifanya majaribio kwa wiki kadhaa katika klabu ya Ligi Kuu Israel mwaka 2010 na baadaye Afrika Kusini katika klabu ya
Supersport United, Bocco alifuzu Supersport baada ya wiki mbili,
lakini Azam FC ikagoma kumuuza kwa sababu ya dao dogo.

Hata hivyo, Msimu wa 2012–13, CRB Ain Fakroun ilishika nafasi ya kwanza katika Professionnelle 2 na
kufanikiwa kupanda Ligi Kuu ya Algeria ijulikanayo kama Professionnelle 1 kwa mara
ya kwanza, kabla ya kushuka tena,
John Raphael Bocco aliyezaliwa Agosti 5, mwaka 1989 amewahi kufanya majaribio Afrika Kusini na Israel, ambako licha ya kuelezwa
alifuzu, lakini biashara haikufanyika.


No comments

Powered by Blogger.