Header Ads

POLISI WAPORWA BUNDUKI - TANGA

Watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wamewavamia na kuwajeruhi askari mwenye
no G 369 PC Mansour na Hv 507 PC Mwalimu, wakiwa doria ya pikipiki ambao walinyang 'anywa silaha mbili aina ya SMG no 14301230 na 14303545 na watu wasio
julikana mkoani Tanga.

Taarifa ya Jeshi hilo kwa vyombo vya habari imesema tukio hilo limetokea Januari 26, 2015
majira ya saa 23 : 30 hrs eneo la barabara 04 jijini humo.

Aidha, mmoja wa majeuhi askari
mmoja no H 507 PC Mansour amejeruhiwa vibaya maeneo mbalimbali ya mwili na amelazwa katika Hospitali ya Mkoa Bombo.

Hata hivyo, Katika uchunguzi wa awali Polisi wamefanikiwa kumtia hatia hatiani mtuhumiwa mmoja,
Ayubu Haule (27 ), fundi Radio Mkazi wa Corner Z Amboni Kiomoni ambaye alikamatwa eneo la tukio akijaribu kutoroka na pikipiki na
mara baada ya kupekuliwa ndipo alipokutwa na mchoro wa ramani unaoonyesha matokeo ya Barabara na kufunguliwa kesi yenye no
TAN/IR /322 /2015.

Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na Jeshi hilo huku timu ya Intel na makachero wa Polisi ikiendelea kufanya doria pamoja na Section 2
za FFU.

Source : Jamiiforum

No comments

Powered by Blogger.