Header Ads

MAMBO SABA (7) YATAKAYO DUMISHA MAHUSIANO


Hakuna binadamu asiyefahamu nini
maana ya mapenzi na kama wapo basi ni
wachache sana na wanaweza kuwa
hawafahamu kwa maneno lakini
kivitendo wanakuwa wanafahamu aidha
kwa kuona, kusikia na hata kwa wao
wenyewe kushiriki kwenye mapenzi
hayo.
Na hakuna binadamu yeyote asiyependa
kupenda au kupendwa, wote tunapenda
kupenda na pia tunapenda kupendwa in
return. Na siku zote ukipenda na
usipopendwa pale unapopenda huwa
inakuwa ni huzuni sana na wengine
hufikia hatua mbaya sana za kufikiria
mengine mengi tu ya hatari pale mapenzi
yanapokuwa machungu kwao.
Hii ndio sababu wengi wetu huwa
tunakaa pale tunapoona kweli kuna
mapenzi na si kukaa pale ambapo
unaona unadanganywa au kuzungushwa
kila siku. Lakini kuna wakati tunaweza
kujikuta hata pale tunapopenda na
kupendwa pia panaharibika baada ya
muda na kunakuwa na ugomvi na
kukosa maelewano baina yenu na wakati
mwingine usifahamu kwa nini
hamuelewani au ukaelewa lakini ukakosa
njia za kutatua.
Zifuatazo ni baadhi tu ya njia mbalimbali za
kufanya ukae na mpenzi wako kwa muda
mrefu kwenye mahusiano na mkafurahia
mapenzi yenu popote pale mtakapokuwa na
mtakapoishi.

1. KUWA NA MUONEKANO CHANYA (POSITIVE IMAGE) KWA MPENZI WAKO.
Ukiwa Ni Mtu Wa Kuangalia Mabaya/Kasoro
Sana Kwa Mpenzi Wako Kuliko Mazuri Yake
Hautakuja Kukaa Kwenye Relationship Kwa
Muda Mrefu Hata Siku Moja...Utaendelea
Kubadilisha Wanaume/Wanawake Kila Siku
Na Mwisho Wa Siku Utajiona Huna Bahati
Kwenye Mapenzi Na Wakati Unayeyaharibu
Mapenzi Yako Ni Wewe Mwenyewe...Hakuna
Asiye Na Kasoro (Ukiwemo Wewe
Mwenyewe). Kwa Hiyo Muonyeshe Mpenzi
Wako Mapenzi Bora Na Umrekebishe Pale
Anapokosea Bila Kuwa Na Lawama Mara
Kwa Mara, Kuna Makosa Mengine Ni Madogo
Sana Na Unaweza Kuyarekebisha Kwa Kukaa
Chini Na Mpenzi Wako Mkayamaliza Kwa
Dakika 5 Tu Lakini Wengine Huwa Issue
Kubwa Kwao Na Kusababisha Mwisho
Mbaya.

2. SAMEHE NA KUSAHAU.
Unapomsamehe mpenzi wako kwa kosa
lolote alilokosa basi hakikisha umemsamehe
kiukweli na ujitahidi kusahau kosa
alilotenda itasaidia uwe na amani ya moyo
zaidi kuliko kumsamehe kwa usoni tu lakini
moyoni ukawa na Donge bado, hii hupelekea
kupunguza mapenzi kwa kiasi Fulani kwake
na kujikosesha furaha ya
mapenzi.Anapokosea siku nyingine
usimkumbushe kosa lake la nyuma kwa
sababu itamfanya ajione mwenye huzuni na
ajione kuwa hakusamehewa.

3. MPE NAFASI/UHURU MPENZI WAKO.
Mnapokuwa kwenye mahusiano
jitahidini kwa hali na mali kupeana
nafasi/uhuru kwenye mambo mengi hasa
yale ya kitaaluma zaidi na
kimaisha.anapokwambia yupo kwenye
kikao cha kikazi jaribu kumuelewa na
umpe support ya kutosha kwenye kazi
zake au biashara zake au hata masomo
yake.usipende sana kulalamika pale
anapochelewa kurudi kazini au kutoka
kwenye biashara zake bali mpokee kwa
upole na baada ya kupumzika ndipo
muulize kwa upole na kimahaba zaidi
kwanini siku hizi anachelewa sana
kurudi au kwenye biashara zake au
shuleni tofauti na zamani.Hii itajenga
zaidi kuliko kubomoa kwa kulalamika na
kupayuka mbele yake na huku yeye
akiwa hata hajapumzika na itamfanya
siku nyingine aione nyumba chungu kitu
ambacho si kizuri kwenu wote wawili.

4. KUWA MBUNIFU KWENYE MAPENZI.
Napozungumzia ubunifu hapa nakuwa
simaanishi kwenye upande mmoja tu wa
kwenye yale mambo yetu ya chumbani,
hapana. Hapa namaanisha ubunifu
kwenye mambo mengi ndani na nje ya
nyumba, jitahidi mara kwa mara kubuni
vitu vipya vitakavyofanya azidi
kukupenda na kukuona kama mpya
kwake kila siku. Kama amezoea kupata
zawadi za aina Fulani kutoka kwako basi
jitahidi siku moja kumbadilishia zawadi
kutegemea na unavyomfahamu mpenzi
wako anapenda nini na nini. Hakuna
anayemjua mpenzi wako zaidi kuliko
wewe kwa hiyo lazima ujue ukifanya nini
kwake na kwa wakati gani atafurahia na
kujivunia kuwa nawe.

5. USIPENDE KUMFANYIA KITU UNACHOONA AKIKUFANYIA WEWE UTAKOSA FURAHA.
Hakuna kitu kibaya kwenye
mapenzi kama kukosa mapenzi
uliyoyategemea kutoka kwa mpenzi
wako. Kama unaona mpenzi wako aki-
cheat utaumia sana basi hata yeye siku
uki-cheat ataumia tena inawezekana
kuliko wewe utakavyoumia. Usimfanyie
kitu amabacho wewe hupendi kufanyiwa
hata siku moja.

6. MFANYE AJIVUNIE KUWA NAWE.
Hakikisha katika mapenzi yenu kila siku
unamfanya mpenzi wako ajivunie kuwa
nawe na hakikisha humfanyi ajute kwa
kukuchagua wewe miongoni mwa wote
aliowaona. Usijidanganye hata siku moja
kuwa kwa kumpata tu na kwa yeye
kukupenda basi hajaona mwingine wa
kuweza kuwa naye. Wapo wengi sana
anaoweza kuwa nao lakini amekuchagua
wewe katika hao wote, kwa hiyo
usimfanye aanze kuwafikiria wale
wengine wanaomfuatilia kila siku na
kumsumbua.Ukianza kumwacha aanze
kuwafikiria wengine aidha kwa wewe
kuwa unamkosesha amani ya mapenzi
kila mara au kwa mengine mabaya ndani
ya mapenzi basi ipo siku utaishia pabaya.

7. MSAIDIE KWA KHALI NA MALI.
Kwenye mahusiano huwa kuna kupanda
na kushuka miongoni mwa wapenzi na
hasa kiuchumi na hata kisaikolojia.
Hakuna kitu kizuri kwenye mapenzi
kama mtu kupata tatizo na akasaidiwa na
mpenzi wake katika hali ambayo
hakuitegemea, namaanisha mpenzi wako
akipata tatizo lolote hakikisha wewe ndo
unakuwa wa kwanza kulifahamu na
kulifanyia kazi. Sio matatizo yote
yanamalizwa kwa pesa so hata ushauri
na kumpa mawazo chanya inasaidia sana
na kumfanya awe na furaha kuwa
nawe.Kama unampenda usione tabu
kumsaidia kwa kuogopa kuonekana eti
unahonga, huyo ni mpenzi wako kwa
hiyo jiamini na umpe kile anachostahili
kusaidiwa na mpenzi wake.
Yapo mambo mengi sana ambayo kama
mkiyafanya kwenye mapenzi basi
uhusiano wenu utakuwa wa kudumu na
wenye furaha sana ingawa hapa
nimezungumzia kwa uchache sana lakini
nina imani itasaidia sana kwa wote walio
kwenye mahusiano .
Mapenzi hayana ndumba au limbwata
hata siku moja, unapoona wapenzi wengi
wana furaha kwenye mapenzi yao ni kwa
sababu wanavumiliana kwa mengi na
kusameheana kwa mengi.

No comments

Powered by Blogger.