Header Ads

Lil Wayne Kumpeleka Birdman Mahakamani

Wayne anadaiwa kuwa na mpango wa kumpeleka bosi wake mahakamani baada ya njia za kawaida kumaliza tofauti zao kushindikana.

Mtandao wa TMZ umedai kuwa wawili hao walijaribu kuyamaliza kifamilia zaidi lakini sasa Weezy amedhamiria kumshtaki Birdman ili atoke kwenye uongozi wa Cash Money Records.

“I’m a one-man army / And if them
n**as comin’ for me, I’m goin’ out like Tony / Now I don’t want no problems, I just want my money. All I got is Young Money, no more Cash, ni**a,” anarap.

Aidha, Wayne anasema Birdman amekiuka mkataba wao kwa kuhodhi album ya Tha Carter V na amesema anamdai Birdman dola milioni nane kama advance ya album hiyo.

Hata hivyo, Birdman anashikilia msimamo wake kuwa ataitoa album hiyo katika muda anaotaka yeye na sio vile anavyotaka Weezy.

Pia, Rapper huyo wa Young Money
ataendelea kurekodi na kuachia
nyimbo zake nje ya Cash Money,
Kwenye wimbo ‘Coco’ uliopo kwenye
mixtape yake mpya, Sorry 4 the Wait 2, Weezy amewachana Cash Money.

Source; TMZ

No comments

Powered by Blogger.