Header Ads

COASTER LAGONGANA USO KWA USO NA LORI, WATU 40 WANUSURIKA KUFARIKI - DAR

Watu zaidi ya 40 wamenusurika kifo huku mmoja akikatika viungo vya miguu na wengine kujeruhika vibaya baada ya lori moja la jeshi kugongana uso kwa uso na gari la abiria aina ya COSTA la Ubungo -Tegeta eneo la Tegeta jijini Dar es salaam.

Tukio hilo limetokea leo Tegeta huku baadhi ya mafundi gereji wa Tegeta wakijaribu kutumia vifaa maalumu kukata mabati ya magari kwa nia ya kunasua baadhi ya majeruhi walionasa ndani ya COASTA hiyo kusuru abiria walioonekana
kunasa katika vyuma vya magari
hayo.

Aidha, Baadhi ya mashuhuda na dereva wa COSTA pamoja na kuomba eneo la kibaoni kuweka njia ya mzunguko maarufu kama ROUND ABOUT kwa lengo la kuepusha madereva wanao lazimika kugeuza kwa dharura katika njia kuu maarufu kama UTAN kutokana na njia hiyo kukosa fursa ya kugeuza endapo kuna ulazima wa kufanya hivyo.

Pia wamemtupia lawama Dereva wa Lori kama msababisha ajali kwa kukosa hekima ya kuchukua tahadhari kabla ya kufanya hivyo.

Naye, Kamanda wa polisi mkoa kipolisi Kinondoni Kamilius Wambura amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akieleza kutoa taarifa mara baada ya uchunguzi kufanyika

No comments

Powered by Blogger.