Header Ads

RAIS SHEIN AMPONGEZA MANYIKA, AMTAKA AONGEZE BIDII ATAKUWA BORA ZAIDI

RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein jana alimpongeza kipa wa Simba SC, Peter Manyika na kumtaka aongeze juhudi aje kuwa
bora zaidi baadaye.

Rais Shein alimpa pongezi hizo Manyika wakati anamvisha Medali ya ushindi wa Kombe la Mapinduzi kufuatia kuifunga Mtibwa Sugar kwa
penalti 4-3 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.

Rais amenipongeza wakati ananivalisha Medali, akaniambia niongeze juhudi nije kuwa
kipa bora zaidi,”alisema Manyika jana alipokuwa kuwa akizungumza na vyombo vya habari.

Hata hivyo, Manyika amedaka mechi zote za Simba SC Kombe la Mapinduzi kuanzia hatua ya makundi na kufungwa bao moja tu katika mchezo wa kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar, Wekundu wa Msimbazi wakilala 1-0, Angeweza kutangazwa kipa bora jana, kama Simba SC ingechomoza na ushindi ndani ya dakika 90, lakini akazidiwa kete na Said Mohamed wa Mtibwa aliyecheza penalti moja
katika matuta.

Aidha, Mtoto huyo wa kipa wa zamani wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Yanga SC, wengi wanamtabiria kuwa mlinda mlango tegemeo la taifa baadaye iwapo ataongeza bidii.

No comments

Powered by Blogger.