SERIKALI YAPIGA MARUFUKU WANANCHI KUTUMIA MAJI YA VISIMA - KAHAMA
SERIKALI wilayani Kahama mkoani
Shinyanga imepiga marufuku wananchi wa kijiji cha namba tisa kata ya Bulyanhulu wilayani hapa kutumia maji ya visima pamoja na kuendesha shughuli za kilimo kufuatia kuvuja kwa bwawa la maji ya mgodi wa Dhahabu wa ACACIA Bulyanhulu yanayosadikiwa kuwa na sumu ya Syned.
Akizungumza na wandishi wa Habari mkuu wa wilaya ya Kahama,Benson Mpesya alisema serikali imeamua kupiga marufuku utumiaji wa visima vya maji pamoja na shughuli za kilimo katika kijiji hicho mpaka mpaka baraza la Usimamizi wa mazingira (NEMC) itakapomaliza uchunguzi kuhusu kemikali hizo.
Mpesya alisema kufuatia bwawa hilo kujaa maji na kutiririka katika kijiji hicho kilichopo jirani na mgodi huo uongozi wa kampuni ya ACACIA iliamua kufunga mabomba sita ya maji kutoka katika mgodi huo kwenda kwenye kijiji hicho huku kwa lengo la kuwasaidia wananchi mpaka hapo uchunguzi utakapokamilika.
Pia, Mpesya alisema kijiji hicho
ambacho kipo ndani ya leseni ya mwekezaji wa kampuni ya hiyo ambapo bado haijalipa wananchi fidia kilikuwa na jumlaya kaya tatu
zenye watu wapatao 27 huku madhara yaliyotokea ni kukauka kwa mazao na maji kubadirika rangi tofauti na yalivyokuwa hapo
awali.
Naye, Afisa usalama wa mgodi
wa Dhahabu wa Bulyanhulu Abdallah Masika akiongea kwa niaba ya msemaji wa mgodi huo alisema kufuatia kutokea kwa
tukio hilo uongozi umeimarisha
miundombinu ya visima na kwamba hali hiyo haiwezikujirudia tena.
Aidha, Bwawa hilo lilianza kutiririsha maji hayo tangu tarehe 9/01/2015 kufuatia mvua kubwa ya mawe iliyonyesha yenye milimita 50 na
hivyo kusababisha bwawa hilo kufurika na maji yake kuelekea katika kijiji jirani cha namba tisa.
Source; Kijukuu cha bibi k blog
Post a Comment