VIJANA WATATU KUTOKA GEITA WALIOKUWA NA LENGO LA KUMUONA RAIS WAKAMATWA DAR
VIJANA watatu wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA, wamekamatwa na polisi eneo la Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam Ijumaa Januari 2, 2014, baada ya jaribio lao la kufanya matembezi kutoka mkoa wa Geita wakielekea Ikulu ya Dar es Salaam kumuona Rais Jakaya Kikwete kufikisha malalamiko yao.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa
Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Jordan Rugimbana, vijana hao watatu, Juma Maganga, Khalifa Selemani na Athanas Michael, walielekezwa na maafisa usalama kumuona yeye DC baada ya
kuwasili kwenye eneo lake la utawala wakitokea Geita, ili awape baraka za kwenda Ikulu.
Hata hivyo, walipofika ofisini
hapo, DC huyo alitaka kujua nini hasa kilichowafanya watembee safari ndefu kama hiyo?.
Naye, DC Rugimbana alisema; "Wameleza kuwa Mosi, Wanataka Kumnuona Rais ili wamueleze kuchukizwa kwao na vitendo vya viongozi kula rushwa na hakuna hatua dhabiti zinazochukuliwa dhidi yao, kukithiri kwa matumizi mabaya ya rasilimali za taifa, kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji dhidi ya raia, na kudai kurejeshwa kwa serikali ya Tanganyika".
Aidha, Baada ya kusikia hayo, DC aliwaeleza kuwa kila Mtanzania anayo haki ya kumuona Rais wa nchi, hata hivyo sio kumuona kiholela bali ni kwa utaratibu
maalum, na kwa kufikia hatua waliyofikia vijana hao, tayari walikuwa wamevunja
sheria lakini akawataka wasubiri
awasiliane na wakubwa ili waandaliwe utaratibu wa kumuona Rais.
Pia, vijana hao walikataa na
walipotoka nje ya ofisi ya DC hapo
Kinondoni, walifanya tena jaribio la
kuelekea Ikulu na safari hii polisi
hawakufanya masihara, waliwaweka chini ya ulinzi mita chache kutoka taa za kuongozea magari kwenye makutano ya barabara za Morogoro na Kawawa ukiwa uneelekea Kariakoo.
Post a Comment