Header Ads

Theluji Yatishia Marekani

Dhoruba kubwa ya theluji inatarajiwa kuathiri sehemu kubwa ya kaskazini- mashariki mwa
Marekani katika siku mbili zijazo ikianza kupiga maeneo makubwa ya mijini kutoka Washington DC
hadi Boston jumatatu.

Kiwango kikubwa cha dhoruba kilikwepa mji mkuu wa Marekani lakini ilipiga upande wa kaskazini
kwenye majimbo ya New Jersey, New York, Connecticut, Rhode Island na Massachusetts ambapo walitangaziwa hali ya dharura kutokana na theluji.

Mamilioni ya watu waliombwa kukaa nyumbani wakati usafiri wa reli wa Amtrack ulipunguza
huduma za treni katika maeneo yenye shughuli nyingi katika ukanda wa kaskazini mashariki yaani
Northeast Corridor na mashirika ya ndege yalifuta mamia ya safari za ndege katika kujiandaa na hali
ya dhoruba jumatatu usiku hadi jumatano.

No comments

Powered by Blogger.