Header Ads

Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Pili 2014....Ufaulu Waongezeka kwa 3%, BOFYA HAPA KUYAONA


Baraza la Mitihani la Taifa nchini Tanzania NECTA leo limetoa matokeo ya mtihani wa Taifa wa Kidato cha pili mwaka 2014 kwa wanafunzi waliofanya mtihani huo unaowapa fursa ya kuendelea na kidato cha tatu.

Akisoma taarifa hiyo leo kwa waandishi wa habari katika ofisi za NECTA jijini DSM, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Charles Msonde amesema kiwango cha ufaulu kwa mwaka 2014 kimeongezeka kwa asilimia 3.32 kutoka asilimia 89.34 mwaka 2013 hadi asilimia 92.66 mwaka 2014.

Amesema waliosajiliwa kufanya mtihani walikuwa 453,191 lakini waliofanya mtihani walikuwa 405,204 sawa na asilimia 89.40 na kwamba wanafunzi 47,987 sawa na asilimia 10.60 hawakufanya mtihani huo kwa sababu tofauti.

Hata hivyo, Dkt Msonde amesema Jumla ya wanafunzi waliofaulu kwa kupata alama zinazowaruhusu kujiunga na kidato cha Tatu ni 375,434 sawa na asilimia 92.66 ambapo kati yao wasichana ni 195,328 na wavulana ni 180,106. Jumla ya wanafunzi 29,770 sawa na asilimia 7.34 wamefeli kwa kushindwa kufaulu kwa kiwango kinachotakiwa, na hivyo watalazimika kukariri darasa.

Pia, Dkt Msonde amesema kuwa matokeo hayo yamepangwa kwa mfumo Wastani wa Pointi (GPA) ambapo madaraja yamepangwa kwa Distinction, Merit, Credit, Pass na Fail. Jumla ya wanafunzi 180,965 sawa na asilimia 44.66 wamefaulu kwa madaraja ya juu (Distinction, Merit na Credit).

Ametaja ufaulu kwa kila daraja kuwa ni kama ifuatavyo Distinction wanafunzi 35,656 sawa na asilimia 8.8 Merit wanafunzi 57,945 sawa na asilimia 14.30 Credit wanafunzi 87,364 sawa na asilimia 21.56 Pass wanafunzi 469 sawa na asilimia 47.99.

Kwa upande wa ufaulu katika masomo, Dkt Msonde amesema kuwa somo lililoongoza kwa ufaulu ni History ambalo wamefaulu kwa asilimia 90.71 na somo lenye ufaulu mdogo zaidi ni Basic Mathematics ambalo ufaulu wake ni asilimia 18.15.

Masomo yenye ufaulu mzuri ni Civis, History, Kiswahili na English ambapo ufaulu ni asilimia 84 yakifuatiwa na Geography, Biology na Book- keeping yenye ufaulu wa kati ya asilimia 50-70 na masomo yenye ufaulu wa chini ni Chemistry, Basic Maths, Physics, Commerce na Agriculture ambayo ufaulu wake ni chini ya asilimia 50.

Amesema katika baadhi ya masomo, baadhi ya wanafunzi wameonesha umahiri kwa kufaulu kwa kupata alama 100%.

Masomo hayo ni Englishi wanafunzi 41 Basic Maths wanafunzi 9 Biology mwanafunzi 1 na Book keeping mwanafunzi mmoja.

Aidha, Ameipongeza serikali kwa kutekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) kwa madai kuwa ndiyo sababu ya matokeo haya kuwa mazuri lakini ametaka juhudi ziendelee kufanywa katika masomo yenye ufaulu wa chini.

Bofya hapa kutazama matokeo; NECTA

No comments

Powered by Blogger.