Header Ads

RUSHWA HOSPITALI YA WILAYA KIKWAZO CHA WANANCHI KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF) - KAHAMA

IMEELEZWA kuwa ubadhilifu pamoja na Rushwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga ni mojawapo ya sababu zinazochangia Wananchi kutokuwa na imani na huduma zinazotolewa katika Hospitali ya Wilaya pamoja na kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF).

Yalisemwa hayo juzi na Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (PCCB) Wilaya ya Kahama Enock Ngailo katika kikao cha Wadau wa Afya wa Halmashauri ya
Wilaya ya Msalala kilichofanyika katika ukumbi wa PHN Mjini Kahama.

Ngailo alisema, "kutokana na kuwa na vitendo hivyo katika Hospitali ndio kumesababisha baadhi ya wananchi kukimbia huduma zinazotolewa katika Hospitali hiyo na kuhamia kwa waganga wa kienyeji hali ambayo ni mbaya hasa kwa jamii ya akinamama na watoto".

Aidha, Awali akifungu kikao kikao hicho cha wadu wa Afya, Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya aliwataka watumishi wa idara hiyo kukhakikisha kuwa wanaimarisha
mfuko wa bima ya afya ili mwananchi awe na uhakika wa kupata dawa na matibabu kwa wakati muafaka pindi anapoumwa.

Hata hivyo, Mpesya alisema kuwa anajua kuwa eneo la kuhusu madawa linahitaji gharama lakini
aliwataka kuwaeleza wananchi kuwa ukiwa na bima ya afya famia inakuwa na uhakika wa kupata huduma ya matibabu kwa wakati.

Source; Kijukuu blog

1 comment:

  1. Ndugu wana Blog ya AFRICAN POWER MIX nimegundua kunaufupisho sana wa taarifa kiasi kwamba nakosa logic ya Tatizo unaposema WAMAMA NA WTOTO wamekimbilia tiba asili kwa sababu ya rushwa. nakubali rushwa ni tatizo sio BIMA TU hata maeneo nyeti ya nchi lakini DAWA NA VIFAA STAHIKI VIPO? nachofahamu ni kwamba WANANCHI WANAHITAJI HUDUMA , BIMA NI MFUMO NAUFAHAMU VIZURI NA UNAFANYA VIZURI. SHIDA NI DAWA NA VIFAA PENGINE VIMECHAKACHULIWA NDIO WANAKOSA MATIBABU. Naomba tuchunguze upya hili tatizo coz linagusa MAISHA YETU. hebu tujiulize vitanda vipo vya kutosha? Dawa zipo? Vifaa vipo? Wataalamu wapo? BIMA SIO ISSUE SANA!

    ReplyDelete

Powered by Blogger.