Header Ads

Utafiti: Wanaume ni wabinafsi zaidi kuliko wanawake

Wanaume hupendelea kuwa wabinafsi zaidi kuliko wanawake, utafiti wa Marekani umeeleza baada ya kuchambua taarifa za miongo mitatu kutoka kwa watu zaidi ya 475,000.

Tafiti hizo zilifanya kwa makundi mbalimbali umri na vizazi, kilieleza Chuo Kikuu cha Buffalo, na kuonyesha kuwa ubinafsi una faida na hasara zake.

“Ubinafsi unahushishwa na tabia fulani mbaya, ikiwemo kushindwa kuhimili mahusiano ya muda mrefu, tabia mbaya na hasira,” alisema mwandishi Emily Grijava, profesa msaidizi wa oganaizesheni na maliasili watu katika Chuo Kikuu hicho.

Wakati huo huo, ubinafsi unaonekana kukuza kujiamini, kuhimili hisia na hata kuwa kiongozi.”

No comments

Powered by Blogger.